Bondia Rodi Josephat wa Moshi, Kilimanjaro |
Klabu ya Ndondi ya
Mkoa wa Kilimanjaro imesema kifungo kilichokuwa kikiwazuia kuandaa mapambano
mkoani hapa kinakaribia kufika mwisho baada kukamilisha usajili wa klabu hiyo.
Akizungumza na JAIZMELA
mwanamasumbwi Rodi Josephat amesema kwa muda mrefu walikuwa na kikwazo cha
kuandaa mapambano ya ngumi kama ilivyo mikoa mingine lakini kwa sasa
wamefanikiwa baada ya hatua za usajili wa klabu hiyo kuwa katika hatua za
mwisho.
“Tulishindwa kuandaa
mapambano kwasababu tulikuwa hatujasajiliwa na shirikisho la ndondi, kwa sasa
tumefikia hatua nzuri tulianzia wilayani, kisha mkoani na imeshafika taifa
ambako tunaamini ikirudi tutakuwa rasmi tunaweza kuandaa mpambano yetu
wenyewe,” amesema Rodi.
Mwanamasumbwi huyo
ameongeza kuwa sehemu yao ya mazoezi iliyopo mjini Moshi ilizuiliwa kwa muda
kutokana na kushindwa kutambulika na uongozi wa mkoani hapo hali ambayo
iliathiri mwenendo wa mchezo huo mkoani hapo.
Aidha Rodi amewataka
wanamasumbwi mkoani hapo kujiandaa vya kutosha kwa ajili ya mapambano
yatakayokuwa yakifanyika baada ya kukamilisha usajili huo.
Hata hivyo amewataka
wadau waliokuwa wakijitokeza kwa kudhamini mapambano ya ndondi kurudi tena
ikiwa ni sehemu ya kuuendeleza mchezo huo.
STORY & PHOTO BY: Jabir Johnson
EMAIL: jabirjohnson2020@gmail.com
DATE: Machi 23, 2020
0 Comments:
Post a Comment