Machi 11, 1978 alizaliwa mwanasoka wa zamani wa Ivory Coast na klabu ya Chelsea Didier Drogba.
Nyota huyo alikuwa akihudumu katika nafasi ya ushambuliaji. Drogba anasalia kuwa mfungaji bora wa zama zote wa Ivory Coast.
Alifahamika zaidi alipokuwa katika klabu ya Chelsea ambako alifunga mabao mengi kuliko mchezaji yeyote wa kigeni na hadi sasa anashikilia nafasi ya nne kwa kufunga mabao mengi katika historia ya klabu hiyo.
Drogba aliwahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka mara mbili alifanya hivyo mwaka 2006 na 2009. Alizaliwa mjini Abidjan nchini Ivory Coast.
Maisha yake ya soka alianza mtaani na timu za vijana.
Baada ya kucheza katika timu za vijana, akiwa na umri wa miaka 18 alitua katika klabu ya Le Mans ya Ufaransa iliyokuwa ligi daraja la pili nchini humo.
Drogba alisaini mkataba wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 21. Msimu wa 2002-2003 alifunga mabao 17 akiwa na klabu ya Guingamp iliyokuwa Ligue 1.
Olympique Marseille ilimuona Drogba na akiwa hapo msimu wa 2003-2004 alifunga mabao 19 akiongoza katika klabu hiyo kwa ufungaji pia Drogba aliisaidia Marseille kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Katika majira ya joto ya 2004, Drogba alitua klabu ya Ligi Kuu ya England akienda Magharibi mwa London katika klabu ya Chelsea kwa rekodi ya klabu pauni milioni 24, na kumfanya mchezaji wa gharama kubwa zaidi wa Ivory Coast katika historia.
Katika msimu wake wa kwanza alisaidia klabu kutwaa taji la Ligi Kuu kwa mara ya kwanza katika miaka 50, na mwaka baadaye alishinda jina lingine la Ligi Kuu.
Mwezi Machi 2012, alikuwa mchezaji wa kwanza wa Kiafrika kufunga mabao 100 ya Ligi Kuu, na pia akawa mchezaji pekee katika historia ya kutinga fainali nne za Kombe la FA mwaka huo huo.
Pia alicheza katika fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2012, ambapo alifunga bao katika dakika ya 88 dhidi ya Bayern Munich na kutwaa taji hilo. Drogba amewahi kuhudumu na Galatasaray, Shanghai Shenhua. Montreal Impact na Phoenix Rising.
Aliitumikia timu ya taifa kutoka mwaka 2002 hadi 2014 akiifungia mabao 65. Aliiongoza Ivory Coast kwenye Kombe la Dunia la 2006. Alikuwa sehemu ya timu ya Ivory Coast ambayo ilifika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2006 na 2012.
Mnamo Agosti 8, 2014, alitangaza kustaafu kutoka kwa soka ya kimataifa akiwa amefunga mabao 210 katika mechi 497.
0 Comments:
Post a Comment