Mwanzilishi na mwanachama wa zamani wa kundi maarufu la muziki wa reggae Ulimwenguni la Israel Vibration Albert 'Apple Gabriel' Craig amefariki dunia Jumatatu ya Machi 23, 2020. Tarehe rasmi ya kuzikwa bado haijawekwa bayana.
Imeelezwa chanzo cha kifo chake ni magonjwa mchanganyiko lakini sio ugonjwa Corona kama wengi walivyodhani.
Katika ukurasa wa facebook wa Roots Radics' Flaba Holt iliandikwa kwamba Apple Gabriel hali yake ya kiafya haikuwa nzuri kwa muda mrefu hadi mauti yalipomkuta.
Apple Gabriel amekuwa akipigania uhai wake kutokana na maradhi ya Polio tangu akiwa mmtoto na mwili wake haukuwa katika hali nzuri huku ripoti zikisemma miaka 10 iliyopita alikuwa amedhoofu na hali ya kimaisha haikuwa nzuri kwake.
Mara ya mwisho kuonekana katika mitandao ya kijamii hususani Facebook ilikuwa ni Machi 7 mwaka huu ambapo alikuwa akizungumzia namna kiharusi kilivyomfanya hata upande mmoja wa mwili wake kupooza huku akiruhusiwa pasipo kufahamu mahali sahihi pa kwenda.
Maisha ya nyota huyo hayakuwa mepesi hata kidogo, aliendelea kupanda na kushuka baada ya kuachana na Israel Vibration mnamo mwaka 1997.
Alianza vizuri katika maisha yake ya kuongoza uimbaji (solo career) albamu yake ya Another Moses ya mwaka 1999 ilipokelewa vema.
Pia alifanya kazi na wasanii wengine na bendi kadhaa wakiwamo Groundation or Jahcoustix. Haikutosha aliopanda katika matamasha jukwaani kama mwaka 2009 nchini Israel.
Hata hivyo alipambana hadi kufikia kilele cha mafanikio yake pale alipotoa albamu yake iliyofahamika kwa jina la Teach Them Right mnamo mwaka 2010. Licha ya yote hayo bado hali yake ya kiuchumi ilikuwa ngumu akiishi kama yatima na wakati mwingine alikosa hata pesa za kurekodi.
Hatua hiyo ilimfanya aumie moyo kwani nyimbo alizokuwa nazo moyo ziliishia kuumiza moyo wake. Wengi wataendelea kumkumbuka Apple Gabriel kutokana na kipaji chake alichokuwa nacho.
Msanii wa muziki wa reggae Heather Augustyn aliandika, " Apple Gabriel alikuwa na maisha magumu. Alikuwa akiugua kwa njia nyingi.
Siku zake Apple Gabriel hapa duniani zilikuwa ngumu. Lakini moyo wake wa ushujaa na maneno yake yalimfanya Apple Gabriel kuwa mpole na imara, mcheshi na mtu makini, mbunifu na mzalishaji. Alikuwa mwanamuziki kweli kweli."
Baadhi ya nyimbo maarufu na kali wakati akiwa na Israel Vibration We A De Rasta, Why You So Craven, Oh Jah Solid Rock, Mud Up, Rude Boy Shuffling, Friday Evening na Walk The Streets of Glory.
Apple Gabriel amefariki dunia tarehe ambayo miaka 21 iliyopita yaani mwaka 1999 aliachia albamu ya Another Moses. Alijiunga na Israel Vibration mnamo mwaka 1975.
Walianzisha kundi hilo akiwa na wenzake Lascelle ‘Wiss’ Bulgin na Ccil ‘Skeleton’
Spence ambao sauti za watatu hao zilifanya kundi hili ling’are. Walitoa albamu
ya kwanza iliyofahamika kwa jina la ‘The Same Song’ mnamo mwaka 1978
Diskografia ya Apple Gabriel
(1978-1997)
Albums:
.1978 - The Same Song
.1978 - The Same Song Dub - [Reissue: "Israel Dub (Same Song Dub and Unconquered Dub)" 1991 and "Same Song + Dub" 2000]
.1980 - Unconquered People - (Reissue "Survive" 1995 and "Practice What Jah Teach" 1999)
.1980 - Unconquered People Dub - [Reissue: "Israel Dub (Same Song Dub and Unconquered Dub)" 1991].
.1981 - Why You So Craven
.1983 - Live At Reggae Sunsplash (The Gladiators & Israel Vibration)
.1988 - Strength Of My Life
.1990 - Praises
.1990 - Dub Vibration (Israel Vibration In Dub) - (Includes Dub Versions of "Strength Of My Life" and "Praises").
.1991 - Forever
.1992 - Vibes Alive
.1993 - IV
.1994 - IV D.U.B. - (Includes Dub Versions of "IV" and "Forever")
.1995 - On The Rock
.1995 - Dub The Rock
.1996 - Free To Move
.1997 - Live Again!
2) Apple Gabriel - Discography: (Solo Works)
Albums:
.1999 - Another Moses
.2002 - No Racism (Live From Eugene, Oregon)
.2010 - Teach Them Right
EPs:
.2001 - Give Me M.T.V. - (Ep with 4 Tracks) - (Unreleased Tracks)
Compilation/Best of:
.1985 - Israel Vibration Meets Cocoa Tea (Cactus label)
.1997 - RAS Portraits (Ras label)
.2000 - Power Of The Trinity (3 Cd Set) - (Ras label and Sanctuary label)
.2005 - Cool And Calm (Ras label)
.2005 - This Is Crucial Reggae (Sanctuary Records label)
.2010 - Feelin Irie (Continental Record Services label)

0 Comments:
Post a Comment