Machi 24, 2012 nyota wa soka wa Ureno Cristiano Ronaldo alifikisha mabao 100 katika ligi kuu ya soka nchini Hispania (La Liga) wakati huo akiwa na klabu ya Real Madrid.
Bao hilo la 100 lilimpa rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kuifikia rekodi hiyo ndani ya muda mfupi katika historia ya klabu hiyo.
CR7 kama ambayo amekuwa akifahamika na wengi katika ulimwengu wa soka, ulikuwa ni msimu wake wa tatu katika La liga alipojiunga na Los Blancos akitokea Manchester United kwa ada ya pauni milioni 80 mnamo Julai 2009.
Alifunga mabao 26 katika msimu wake wa kwanza, msimu uliofuata alifunga mabao 40. Licha ya kufanya vizuri msimu huo lakini Real Madrid ilisalia kushika nafasi ya pili ya msimamo wa La liga nyuma ya Barcelona waliotwaa taji la La liga.
Msimu wa 2011-12 alifunga mabao 33 katika mechi 28 alizocheza na kufanya mabao kwa misimu yote tangu atue ifikie 99 na msimu huo Real Madrid ilikuwa kileleni mwa La liga. Mechi iliyokuwa inafuata katika La liga ilichezwa katika dimba la Santiago Bernabeu dhidi ya Real Sociedad katika dakika ya sita ya mchezo Madrid walipata uongozi kupitia Gonzalo Higuain.
Baada ya hapo katika dakika ya 32 ya mchezo Cristiano alipokea mpira kutoka kushoto na aliukimbilia kwa kasi katika safu ya ulinzi na kumtungua linda mlango akimpeleka upande wa kulia katika mlingoti wa mbali na mpira ulikwama wavuni.
Bao lake la 100 katika La liga ni mara bada ya kucheza mechi 92 hivyo kuvunja rekodi ya Ferenc Puskas aliyecheza mechi 105 kufunga mabao 100. Hata hivyo hakuweza kufikia rekodi ya Oviedo Isidro Langara alifanya hivyo kwa mechi 90.
Baada ya mchezo huo Cristiano alifunga bao la pili katika ushindi wa mabao 5-1 na msimu huo Real Madrid ilitwaa taji la La liga.

0 Comments:
Post a Comment