Friday, March 6, 2020

Tim Howard mlinda mlango aliyeweka rekodi EPL

Machi 6, 1970 alizaliwa mchezaji wa soka wa Kimataifa wa Marekani Timothy Matthew Howard maarufu kama Tim Howard ambaye alikuwa akihudumu kama mlinda mlango. 

Tim Howard ni miongoni mwa wachezaji wakubwa katika historia ya soka la Marekani. 

Howard alitajwa katika kikosi cha Ligi Kuu ya England msimu wa 2003-04. Mnamo mwaka 2009 alitunukiwa tuzo Golden Glove ya Kombe la Shirikisho la FIFA. 

Howard alizaliwa North Brunswick, New Jersey akiwa ni mtoto wa dereva Mmarekani mweusi na mama yake alikuwa mwenye asili ya Hungaria Esther Fekete ambaye alikuwa mfanyakazi wa kusambaza bidhaa kwa wateja. 

Wazazi wake waliachana wakati Howard akiwa na umri wa miaka mitatu. Howard akaanza kuishi na mama yake. 

Akiwa mtoto aliwahi kupata maradhi ya  Tourette na OCD akiwa darasa la sita.

Alianza maisha yake ya soka akiwa na New Jersey Imperiak kabla ya kwenda zake MetroStars. 
Uchezaji wake ulizivuti klabu za nchini England ambapo Manchester United ilifanikiwa kudaka saini yake mnamo mwaka 2003. 

Alipata mafanikio makubwa akiwa Manchester United pale aliposhinda Ngao ya Jamii mwaka 2003, Kombe la FA msimu wa 2003-04 na Kombe la Ligi 2005-06. 

Nafasi yake ilikuja kuzibwa baadaye na Mholanzi Edwin van de Sar na Howard akatolewa ka mkopo kwenda Everton ambako huko aliweka mizizi katika kikosi cha kwanza hatimaye Toffees wakamsajili moja kwa moja mnamo mwaka 2007. 

Januari 4, 2012 Howard alifunga bao la kwanza la kimataifa katika mchezo wa ligi Kuu nchini England dhidi ya Bolton Wanderers akiweka rekodi ya kuwa mlinda mlango wa nne kufunga katika ligi kuu nchini England. 

Baada ya maisha ya soka nchini England, Howard alirudi zake nchini Marekani katika Ligi Kuu ya Marekani (MLS) ambapo alirudi na kuhudumu na Colorado Rapids. 

Howard ndiye mlinda mlango aliyecheza mechi nyingi katika timu ya taifa ya Marekani akicheza mechi 121 tangu mwaka 2002 hadi alipostaafu mwaka 2017. 

Katika Kombe la Dunia mwaka 2006 nchini Ujermani hakucheza mchezo hata mmoja akisalia kuwa mchezaji wa akiba. 

Mwaka mmoja baadaye alikuja kuwa mlinda mlango tegemeo wa timu ya taifa. 

Alianza kung'ara katika michuano ya Mabara mwaka 2009 ambapo Marekani ilifika fainali dhidi ya Brazil na kuishia nafasi ya pili ya mashindano hayo. 

Howard alicheza katika Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini na 2014 nchini Brazil. 
Marekani iliishia katika hatua ya 16 kwenye mashindano yote mawili. 

Katika Kombe la Dunia aliweka rekodi ya kuwa mlinda mlango aliokoa hatari nyingi zaidi katika lango lake. 

Alifanya hivyo katika mchezo dhidi ya Ubelgiji akiokoa michomo 15.


0 Comments:

Post a Comment