Machi 25, 1975 alifariki dunia Mfalme wa Saudi Arabia Faisal bin Abdulaziz Al Saud. Faisal alikuwa ni mtoto wa tatu wa Mfalme Abdulaziz. Faisal alishika madaraka ya kuliongoza taifa hilo la Kiarabu kutoka mwaka 1964 hadi alipouawa na binamu yake 1975. Faisal aliuawa na binamu yake aliyefahamika kwa jina la Faisal bin Musaid.
Mama yake Faisal alifahamika kwa jina la Tarfa ambaye alikuwa ni miongoni mwa familia ya Al ash Sheikh ambayo imewatoa viongozi wengi wa kidini wa Saudia Arabia.
Faisal alionekana kuwa ni mwenye ushawishi katika siasa za kifalme chini ya baba na kaka yake King Saudi akianza kwa kushika wadhifa wa kuwa Waziri wa Mambo ya Kigeni kwa miaka miwili 1930 hadi kifo chake.
Faisal alikuwa crown prince mnamo mwaka 1953 na alipokuwa katika nafasi hiyo alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kukomesha biashara ya utumwa nchini humo. Mnamo mwaka 1964 alifanikiwa pakubwa kumshawishi Mfalme Saud akiwa madarakani kwa msaada wa wanafamilia wengine kwenye uko wa kifame kumteka nyara Grand Mufti Muhammad ibn Ibrahim Al ash-Sheikh.
Faisal alisimamia sera ya ukisasa na mabadiliko katika taifa hilo. Sera zake katika masuala ya kigeni zilikuwa Pan-Islamism, Utaifa wa Palestina na Anti- communism.
Kuna wakati Faisal alijaribu kupunguza mamlaka ya viongozi wa dini ya Kiislamu katika serikali yake. Pia Faisal alipinga vikali uungwaji mkono wa mataifa ya Magharibi katika taifa la Israel.
Kutokana na msimamo wake aliongoza mgomo wa mafuta ambao ulikuja kuzua balaa la Ukosefu wa Mafuta na mgogoro wa mafuta wa mwaka 1973 uliibuka.
Faisal alifanikiwa kulifanya taifa hilo la kifalme kusimamia na lilikuwa maarufu sana kwa raia wake. Hata hivyo licha ya kufanikiwa sana kufanya hayo lakini kulikuwa na mitafaruku ya mara kwa mara hali iliyosababisha kuuawa kwake.
Faisal aliuawa na binamu yake huyo ambaye alikuwa ametokea nchini Marekani.
Mauaji hayo yalifanyika katika eneo la kupumzika ambalo watu mbalimbali humsubiri Mfalme ili aweze kusalimiana nao. Kama ilivyo desturi ya Waarabu wanaposalimiana lazima wakumbatiane na kupigana busu ambapo muuaji naye alikuwa miongoni mwa waliokuwepo hapo.
Faisal alikwenda kumkumbatia binamu yake huyo ambaye alichomoa bastola na kumtandika Mfalme ambapo risasi ya kwanza Faisal alitandikwa chini ya kidevu na ya pili ilikwenda kwenye sikio.
Bodigadi wa Mfalme aliufuta upanga akitaka kummalizia kabisa muuaji huyo lakini Waziri wa Mafuta Zaki Yamani alipiga kelele na kumtaka asifanye hivyo.
Mfalme alichukuliwa haraka na kupelekwa hospitalini ambako madaktari walijitahidi kuokoa maisha yake lakini ilishindikana hatimaye akafa Mfalme Faisal akafariki dunia.
Serikali ya Saudi Arabia iliahirisha shughuli zote na kutangaza siku tatu za maombolezo. Inadaiwa chanzo cha mauaji hayo ni mauaji ya Prince Khalid bin Musaid ambaye alikuwa kaka wa Prince Faisal.
Prince Khalid aliuawa mwaka 1966 kwa kupigwa risasi na kufa papo hapo na askari kutokana na uvamizi alioufanya katika kituo kimoja cha televisheni.
Inadaiwa kuwa kuwa sera za ukisasa na marekebisho yake vilivyokuwa msingi wa utawala wake baadhi ya watu hawakivipenda kwani vilisababisha maandamano yaliyotokana na ujio wa televisheni nchini humo. Ikiwa na maana moja muuaji huyo alitaka kulipa kisasi.
Mwili wa Faisal ulizikwa katika makaburi ya Al Oud huko Riyadh Machi 26, 1975 na aliyepokea mikoba Mfalme Khalid alimlilia sana Mfalme Faisal wakati wa mazishi yake.
Kwa kuwa miongoni mwa watoto wa Mfalme Abdulaziz kulimfanya Prince Faisal apewe majukumu wa kusimamia baadhi ya masuala katika Saudia Arabia.
Baada ya kuuteka mji wa Hail na kuuweka mikononi mwao mnamo mwaka 1922 alipelekwa kwenye majimbo hayo akiwa na askari akali ya 6,000. Alipata mamlaka kamili ya kusimamia eneo lote la Asir hadi mwishoni mwa mwaka huo.
Hapo ndipo Faisal alipoteuliwa kuwa mkuu wa Hejaz mnamo mwaka 1926 baada ya baba yake kuchukua umiliki wa eneo hilo. Wakati akiwa hapo Hejaz alikuwa na mawasiliano na viongozi wa chini kabisa.
Wakati akiwa Waziri wa Kigeni wa Saudia Arabia Faisal alikwenda kuzuru barani Ulaya mara kadhaa ikiwamo Poland mwaka 1932 na Russia wakati huo ikiwa sehemu ya USSR mwaka uliofuata.
Pia aliamrisha kampen za mapambano ya Saudi na Yemen ya mwaka 1934 na Saudia Arabia. Miaka ya 1950 na 1960 kulishuhudia ulimwengu wa kiarabu ukipitia wakati mgumu wa mapinduzi ya kijeshi hali ambayo ilikuwa ikimnyemelea naye katika utawala wake.
Ulishuhudiwa Libya ikipata msukosuko katika mapinduzi yaliyomwingiza madarakani Muammar Gaddafi. Gaddafi alipata nafasi ya kuzuru Saudia Arabia miaka ya 1970 wakati wa utawala wake Faisal.
Katika suala la utumwa, nchini Saudia Arabia haukuwa umekomeshwa hadi alipopitisha sheria ya kuzuia utumwa nchini humo. Mwandishi na Mtangazaji wa BBC wakati huo Peter Hobday ambaye alikaririwa akisema watumwa 1,682 waliachiwa huru kwa gharama za serikali.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa wakati huo Bruce Riedel alisema suala la kukomeshwa kwa utumwani liliibuliwa na Marekani baada ya Faisal kukutana na Rais wa Marekani wakati huo Franklin, Roosvelt mnamo mwaka 1945 na mnamo mwaka 1962 wakati Rais wa Marekani John F. Kennedy alipotembelea Ikulu ya Riyadh na kumshawishi kukomeshwa utumwa.
Katika maisha yake binafsi Mfalme Faisal alioa mara nne na wake zake walitokea katika famili za nguvu za Al Kabir (Al Jawhara bint Saud bin Abdulaziz Al Saud), Al Sudairi (Sultana bint Ahmed Al Sudairi,), Al Jiluwi (Haya bint Turki bin Abdulaziz Al Turki)na Al Thunayan (Iffat Al-Thunayan).
0 Comments:
Post a Comment