Machi 13, 1901 alifariki dunia mwanasheria na mwanasiasa wa Marekani Benjamin Harrison.
Harrison alihudumu katika taifa la Marekani akiwa Rais wa 23 kutoka mwaka 1889 hadi 1893.
Harrison ni mjukuu wa Rais wa tisa wa Marekani William Henry Harrison. Rekodi hiyo nchini Marekani imewaweka kuwa peke yao kushika wadhifa wa urais kwa mjukuu na babu, haijawahi kutokea katika taifa hilo.
Pia Harrison alikuwa kilembwe wa Benjamini V ambaye alisaini Azimio la Uhuru wa Marekani.
Harrison alikuwa muumini wa madhehebu ya Presbitariani na akiwa kana Mzee wa Kanisa huko Indianapolisi na aliweza kuhudumu katika kamati mbalimbali katika kanisa hilo kitaifa.
Alifariki dunia kabla hajapiga kura katika mkutano mkuu.
Harrison alipatwa na mafua mnamo Februari 1901. Alitibiwa kwa njia ya mvuke wenye oksijeni lakini hali yake ilizi kuwa mbaya.
Alifariki dunia kwa kichomi (pneumonia) akiwa nyumbani kwake Indianapolis akiwa na umri wa miaka 67.
Alizikwa katika makaburi ya Indianapolis Crown Hill pembezoni mwa kaburi la mkewe Caroline.
Mkewe wa pili Mary Dimmick Harisson alifariki mnamo mwaka 1948 naye alizikwa pembeni yake.
Harrison alizaliwa Agosti 20, 1833 huko North Bend, Ohio kwa mke wa pili wa John Scott Harrison, Elizabeth Ramsey (Irwin). Harrison alikuwa miongoni mwa watoto wa kumi.
Familia yao ilitokea Virginia ambako mababu zake walikaa huko wakiwa wahamiaji kutoka England. Mababu zake walifikia katika mji wa Jamestown miaka ya 1630.
Kizazi chote cha Harrison ni kutoka England na walihamia Marekani wakati wa mwanzo kati zama za ukoloni.
Harrison aliapishwa Jumatatu, Machi 4, 1889, na Jaji Mkuu Melville Fuller.
Hotuba yake ilikuwa fupi - kuliko ile ya babu yake, William Henry Harrison, ambayo inashikilia rekodi ya kuwa ni hotuba ndefu kwa marais walitawala taifa hilo.
Katika hotuba yake, Benjamin Harrison aligusia ukuaji wa taifa hilo kwa ushawishi wa elimu na dini, alihimiza majimbo ya yanayojihusisha na kilimo cha pamba na maeneo ya madini kupata idadi ya viwanda ya majimbo ya mashariki na kuahidi ushuru wa kinga.
Kuhusu biashara, alisema, "Kama mashirika yetu makubwa yangefuata kwa umakini majukumu yao ya kisheria, wasingelalamika juu ya mapungufu ya haki zao au kuingiliwa na shughuli zao."
Katika maswala ya nje, Harrison alisisitiza tena kufuata Mafundisho ya Monroe kama msingi wa sera za kigeni, huku akihimiza ukisasa kwa Jeshi la Majini. Alitoa ahadi yake kuwa amani kimataifa itatawala na wala hapatakuwa na uingiliaji wa mambo ya serikali za nje.
Wakati wa utawala wake majimbo hayakuwa 50 kama ilivyo sasa, hivyo majimbo sita yalijiunga katika serikali ya Shirikisho wakati wa utawala wake. North Dakota (November 2, 1889), South Dakota (November 2, 1889), Montana (November 8, 1889), Washington (November 11, 1889), Idaho (July 3, 1890) na Wyoming (July 10, 1890).
Harrison ni miongoni mwa marais 19 walioshika dola la Marekani kwa tiketi ya Chama cha Republican; idadi ambayo kubwa huku Democratic wakichukua wadhifa huo mara 14 mpaka sasa.
0 Comments:
Post a Comment