Baada ya Shirika la Afya duniani (WHO) kutangaza kuwa ugonjwa wa Covid-19 kuwa ni janga la kimataifa, kumekuwa na maoni tofauti kuhusu kusambaa kwa virusi hivyo katika bara la Afrika.
Akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) Machi 12 mwaka huu; Dkt. Gideon Mlawa wa Hospital ya Queens huko Mashariki mwa London Romford nchini Uingereza amesema Afrika ina nafuu kutokana na hali ya hewa ya joto ukilinganisha na maeneo mengine dunia.
"Kwasababu nchi nyingi za Afrika hali ya hewa ni joto sana,na virusi vya Corona havina sugu ya kwenye joto, ina maana kwamba hali ya hewa ikianza kuwa na joto katika nchi ambazo zimepata Corona ugonjwa huu utapungua," alisema Dkt. Mlawa.
Hata hivyo Dkt. Mlawa amesema kitendo cha WHO kutangaza Corona ni janga la dunia sio kwa nia mbaya isipokuwa ni kuzitaka nchi mbalimbali kujiandaa na kuweka miundombinu ya kukabiliana.
"Neno pandemic halitumiki kirahisi lakini ili kuziandaa nchi mbalimbali kukabiliana nalo na sio kuwatia hofu," alisema Dkt. Mlawa.
Hadi sasa takribani watu 4,000 wamepoteza maisha duniani kote na karibu nchi 100 zimepata maambukiza ya Covid-19.
WHO ilitangaza juzi Jumatano Machi 11, kuwa Covid-19 ni janga la dunia (Pandemic disease).
STORY BY: BBC
QUOTED BY: Jabir Johnson
EMAIL: jabirjohnson2020@gmail.com
DATE: Machi 13, 2020
0 Comments:
Post a Comment