James Chilongwe akiwa na wanafunzi wa Himo Secondary Scchool |
Kipawa cha kuyasoma mambo kwa upeo mpana na kwa undani zaidi ndicho hasa kinacholeta maana ya usomi hata bila kukaa kwenye dawati au jengo la shule.
Jim Weiss, mtaalamu wa mambo ya simulizi za hadithi, aliwahi kusimulia tukio ya kifo cha Teddy Roosevelt na tukio la Harry Truman kuwa Rais baada yake.
Mtaalamu huyo alielezea wasifu wa Rais Roosevelt, ambaye alitokea katika familia ya kitajiri, na ambaye alipata elimu katika Chuo Kikuu cha Ivy League. Sifa na akili yake vilionekana kuleta mafanikio. Lakini Umma haukumuona Truman kama mtu mwenye uwezo wa kumrithi Rais Roosevelt kwa namna yoyote ile.
Tofauti kubwa kati yao ni kwamba wakati Teddy Roosevelt alisoma Chuo Kikuu, Truman yeye alijielimisha mwenyewe (self-educated). Alikusanya vitabu na vitabu vya historia na akavisoma na kuvisoma.
Yeye, zaidi, alipendelea kusoma historia ya tamaduni za jamii za kale na watawala wake. Katika mahojiano fulani, Truman alitoa sababu za mafanikio yake makubwa ya kidiplomasia kuwa ni kuzirejea taratibu za jamii zilizofanikiwa katika historia.
Alipenda kurejea nyuma na kuoanisha tatizo la sasa la mwanadamu na ufumbuzi wake uliopatikana huko nyuma. Hili ni jambo lililomletea mafanikio.
Hivyo basi ni jukumu la kila mmoja wetu kutambua maana halisi ya elimu. Miongoni mwa mambo ambayo mtu anapokuwa shuleni kwa ajili ya mafundisho ni kufanya ziara mbalimbali ili kuongeza uzoefu.
Machi 14, 2020 ilikuwa siku muhimu kwa baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Himo mjini Moshi, Kilimanjaro kupata fursa ya kuzuru Redio Kili FM iliyopo Soweto mjini humo.
Wakiwa hapo waliongozwa na mtangazaji James Chilongwe kujionea shughuli mbalimbali za Utangazaji katika kituo hicho cha Utangazaji nchini.
STORY & PHOTO BY: Jabir Johnson
EMAIL: jabirjohnson2020@gmail.comMtangazaji wa Kipindi cha Junction Anold Mosha akiwa na wanafunzi wa Shule ya Upili ya Himo Machi 14, 2020. |
Mtangazaji Joshua Mkiramweni akiwa na mmojawapo wa wanafunzi katika Studio za Kili FM Machi 14, 2020 |
Studio za Redio Kili FM mwaka Machi 14, 2020 |
Kutoka kushoto ni Benny Kuzwa (Zangi Koroboi), Joshua Mkiramweni (Daddy B), Eva Ndimara, Fortunata Mallya na Noel Mkufya. |
0 Comments:
Post a Comment