Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) mkoani Kilimanjaro imewataka wafanyabiashara kuwa wazalendo na nchi yao kwa kulipa kodi stahiki kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Hayo yamebainishwa jana na afisa mwandamizi mkuu mamlaka ya mapato tanzania Hamis Lupenja, akiongea wakati wa semina ya kuwajengea uwezo kwa Mameneja wa TRA ngazi za wilaya za mkoa huo iliyofanyika mjini moshi mkoani Kilimanjaro.
Alisema kuwa wafanyabiashara kulipa kodi si utumwa ni moja ya jukumu lao, ulipaji kodi ni jambo muhimu kwa maendeleo ya taifa, hivyo aliwataka wafanyabiashara hao kulipa kodi zao kwa mujibu wa sheria .
Aidha Lupenja alisema ueledi ndani ya mamlaka ya mapato ni kitu cha msingi sana, ili wafanyabiashara wafanye biashara zao bila kificho hali ambayo itawezesha kukusanya mapato mengi zaidi
“Huwezi kukusanya kodi kama maofisa wa TRA hawana weledi lakini endapo watakuwa na weledi uhiari wa ulipaji wa kodi miongoni mwa wafanyabiashara utaongezeka”alisema.
“Dhima kubwa ya mapato ni kukusanya mapato kwa ajili ya nchi, huwezi kukusanya mapato kama huna ueledi, kwa kuanzia maofisa wanaokusanya kodi, wafanyabiashara ni lazima wapewe elimu ili ulipaji kodi uweze ku ongezeka,”.
Alifafanua kuwa ili uweze kukidhi takwa hilo ni lazima utengeneze uwezo wa ndani, ili kusudi wafanye kazi kwa weledi, wakakadirie kodi sahihi kwenye maeneo sahihi , na wafanyabiashara waone kwamba TRA inawajali.
Nae Meneja wa TRA mkoa wa Kilimanjaro Gabriel Mwangosi, alisema wafanyabiashara pamoja na maofisa wa mamlaka hiyo wanatakiwa washirikiane katika kuhakikisha kodi zote zinakusanywa bila kuwepo na upotevu wowote akiwasihi wale wanaohitaji namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) wafike katika ofisi za mamlaka hiyo na wataipata kwa haraka zaidi kwani mifumo ya uendaji kazi imeboreshwa zaidi.
“Walipakodi wengi hawana maswala ya elimu ya mlipa kodi, wapo wengine kwa mawazo yao wanaona biashara flani haipaswi kulipiwa kodi, tunapita na kuwaelimisha, wajibu wa mfanyabiashara ni kulipa kodi inayositahili na asikadiliwe zaidi ya kile kinachostahili wala asilipe pungufu ya kile kinachostahili kulipwa,”alisema Mwangosi.
Aliongeza kusema kuwa “Bado wimbi la biashara ya magendo imeshamiri sana kwenye maeneo ya mipakani hususan mpaka wa Holili na Tarakea na sisi tumekuwa tukipambana nayo kwa kiasi kikubwa na tumeanza kuona kwa kiasi flani magendo yanakwenda yakipungua tunafanya doria usiku na mchana,”alisema.

0 Comments:
Post a Comment