Friday, February 10, 2023

Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi laanika mikakati yake kuwainua wanawake

 

Kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Mwanamke mkoa wa Kilimanjaro inayotarajiwa kufanyika Machi 8 mwaka huu, Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Kilimanjaro, limesema lipo mbioni kufungua Benki ya Wanawake mkoa wa Kilimanjaro ili kuwainua wanawake kiuchumi.

Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Bi. Joyce Ndosi, aliyasema hayo Februari 9,2023, wakati akiwashukuru wajumbe wa Jukwaa hilo kwa  kumwamini na kuweza kumchagua kuliongoza Jukwaa hilo kwa kipindi cha miaka mitatu.

"Mkoa wa Kilimanjaro  unayo mazao mengi ya kibiashara ikiwemo Ndizi, na Parachichi, Kahawa, mazao haya yote yauzwa na wanawake wajasiriamali wadogo, hivyo tukiweza kushirikiana kama jukwaa na kuanzisha kiwanda ambacho kitakuwa kinasindika mazao haya kila mmoja ataweza kunufaika na biashara hiyo,"alisema Ndosi.

Alisema katika kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan Jukwaa hilo litaweza akuwasaidia wajasiriamali  wadogo kujikwamua kiuchumi na kuweza kutimiza malengo yao.

"Ninacho waahidi kwenu ni kuendelea kushirikiana nanyi bega kwa bega na wanawake  wengine katika kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kupitia nyanja mbalimbali,"alisisitiza Bi. Ndosi.

Mwenyekiti huyo aliongeza kusema katika nafasi ambayo ameipata atahakikisha kwamba anakwenda kuwaunganisha wanawake wote wa mkoa huo ili waweze kufanya kazi kwa pamoja hususani kwenye sekta ya kiuchumi ili kila mjasiriamali  aweze kunufaika na biasha yake anayoifanya.

Kwa upande wake Katibu wa Jukwaa la Uwezeshaji  Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Kilimanjaro  Aisha Mmbaga, amesema moja ya mipango mikakati ambayo wamejiwekea ni kuanzisha Benki ya Wanawake pamoja na kuwa na miradi ya kiuchumi ambayo itaweza kuwasaidia  kujiinua kiuchumi moja kwa moja. 

"Wako wanawake wajasiriamali wengi ambao wamekuwa wakijishughulisha na biashara mbalimbali huku changamoto kubwa kwao ni kukosekana kwa mtaji hivyo kuwa na Benki ya Wanawake  itawawezesha kukopeshwa na kuendeleza biashara zao,"alisema Bi.Aisha. 

Sherehe za maadhimisho ya wiki ya Mwanamke mkoa wa Kilimanjaro  yatafanyika Machi 8, mwaka huu Wilayani Same huku akitoa wito kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki siku hiyo.







 

0 Comments:

Post a Comment