Shule ya Msingi Mawenzi iliyopo Manispaa ya Moshi miongoni mwa maeneo zoezi la upandaji miti lilifanyika kuelekea miaka 46 ya kuanzishwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM). |
UTANGULIZI;
NDUGU Wananchi wa Kata ya Mawenzi na vuinga vyake kwanza napenda kuchukua fursa hiikumshukuru Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema na upendo, kumiwezesha kuwa nanyi hii leo.katika zoezi la upandaji wa miti ili kukabiliana na mabadiliko ya taiba nchi,.
Pia naishukuru kwa dhati Serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mhe; Dkt. Samia Suluhu Hassan na chama cha Mapinduzi (CCM) kunipa ridhaa tena ya kuwahudumia wakazi wa kata hii ya Mawenzi.
Vilevile napenda kuwashukuru Makamu wa Rais Dkt. Philip Mapango na Waziri Mkuu Mhe; Kasim Majaliwa (Mb) pia Mstahiki Meya wa Ma ispaa ya Moshi.Injinia Zubery Abdallah Kidumo, kwa miongozo na.maelekezo wanayoyatoa kuhakikisha mangira yanaendelea kutunzwa.
Ndugu Wananchi baada ya maelezo haya ya utangulizi, Sote tunafahamu duniani kwa sasa inahangaika kutafuta suluhisho namna ya kulinda safari hii dhidi ya mabadiliko ya tabia ya nchi, kutokana na matukio mengi ya ukame na mafuriko kupindukia kiwango kinachotakiwa.
Mabadiliko ya tabia nchi yapo na husababishwa haswa na shughuli za kibinadamu, kwa sasa kumekuwa na mkusanyiko wa gesi ya hewa ukaa kwenye mazingira duniani ambako kunahusishwa moja kwa.moja na wastani wa kiwango cha joto duniani.
Shirika la Kimataifa la Mpango wa mazingira (UNEP) linasema asilimia 30 ya idadi ya watu ulimwenguni wanakabiliwa na mawimbi ya joto yanayotokea
Ndugu Wananchi, upandaji wa miti katika mazingira yetu unachangia kwa kiwango kikubwa katika kutunza.mazingira kwa.kuzuia kuenea hali ya jangwa kupitia kuleta mvua na pia kutunza vyanzo vya maji ardhini.
Ndugu Wananchi; Mkoa wetu wa Kilimanjaro sote tunafahamu hapo awali ulikuwa na hali ya hewa nzuri , mvua za kutosha lakini kwa sasa kama mnavyoona hali imebadilika mkoa wetu ulikuwa na misimu miwili ya mvua tulikuwa na mvua za vuli na masika lakini kwa sasa mvua za.vuli.imetoweka kwasababu ya uharibifu wa mazingira na ukataji wa miti hovyo.
Wote mnashuhudia kwa sasa Manispaa yetu ya Moshi, tumeshuhudia mgao wa maji ambao.umeanza leo hii ni miongoni mwa mabadiliko makubwa ya tabia nchi, jambo kama hili halikuwqhi kuwepo katika mazingira yetu.
Ndugu Wananchi, leo tunapanda miti takribani 100 kwa ajili ya kukabiliana na hali mbaya ya hewa katika siku za usoni kama tusipochukua hatua madhubuti jambo la.msingi ni kuitunza , tumeanza leo lakini uangalizi madhubuti unapaswa kuzingatiwa ili miti hii iwe chachu ya kutunza vyanzo vya maji na viumbe wa majini na nchi kavu ambao ni muhimu kwa maendeleo ya taifa letu.
Mimi na wewe ndio chanzo cha yote haya, lakini pia mimi na wewe ndio suluhisho muhimu katika kuirudisha Kilimanjaro ya zamani yenye hali ya hewa nzuri ya kuvutia.
Ndugu wananchi wa Kata ya Mawenzi nihitimishe kwa kusema ili kukabikiana na hali ya hewa na mabadiliko ya tabia nchi inatupasa sote tufanye kwa vitendo sio kuzungumza pekee.
Shughuli za kibinadamu utupaji wa taka zikiwemo za plasitiki zinabadilisha hali ya hewa na mazingira kwa ujumla. Tusaidiane kudhibiti ili kuitengeneza kata yetu Mawenzi, Moshi yetu, Kilimanjaro yetu, Tanzania yetu na dunia kwa ujumla
AHSANTE KWA KUNISIKILIZA.
0 Comments:
Post a Comment