Madiwani wa Moshi mkoani Kilimanjaro wanatarajia kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo wilayani humo Jumamosi ya Tarehe 11 Februari 2023.
Akizungumza
kwenye kikao maalum cha Baraza la Madiwani cha kupitisha mapendekezo ya mwaka 2023-2024, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi Moris Makoi alisema,
“Tumeamua sisi kama madiwani kuvitembelea na kuvitangaza vivutio vyetu vya
ndani na Kauli Mbiu ni "Utalii wa
Ndani Tuanze na Sisi Wenyewe".
Makoi aliongeza
kusema kabla ya kupanga ziara hiyo ya siku moja walipendeza kamati ambayo
ilifuatilia na kuvibaini vivutiovya
utalii kasha kuwasilisha katika vikao
vya halmashauri.
Aidha alitoa
wito wa kila diwani katika eneo lake kuhamasisha utalii wa ndani.
Kwa upande
wake Kaimu Afisa Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira Wilaya ya Moshi Innocent Paulo
alisema, “Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
inavyo vivutio vingi sana ambavyo vingi havijatangazwa ipasavyo … Uwepo
wa mlima mrefu barani Afrika Mlima Kilimanjaro watalii wengi wanakuja kuupanda
mliama huo lakini kama wangevitambua na hivi vingine itasaidia pia kuvitangaza.”
Diwani wa Uru Mashariki Samweli Materu alisema, “Madiwani ndio kichocheo kikubwa cha maendeleo ndani ya kata husika hivyo ziara ya madiwani ina umuhimu mkubwa sana katika kuwahamasisha wananchi kuvitembelea vivutio hivyo,”.
“Kata Uru
Mashariki kwenye kijiji cha Materuni kuna mradi mkubwa wa
"Mnambe" ambayo ni maanguko ya maji, wageni wengi wamekuwa
wakitembelea eneo hilo,”aliongeza diwani huyo.
Madiwani
wa Mbokomu na Kibosho Kati Raphael Materu na Bahati
Mamboma walisema Kamati ilibaini kuwepo
kwa vivutio vyingi ambavyo havitambuliki licha ya kuwepo kwa kuanza ambako
kutahamasisha utalii wa ndani na taarifa zake kuenea kwa Watanzania
Wilaya ya Moshi ina vivutio vya utalii Maporomoko ya Maji ya Materu, Mahandaki, Mti Mrefu barani Afrika uliopo Kidia, Mahali aliponyongewa Mangi Meli katika mti wa Mgunga eneo la soko la Tsuduni.
Maporokomo ya Maji ya Materuni yaliyopo wilayani Moshi. |
Diwani wa Mbokomu Raphael Materu (wa kwanza kushoto) mnamo Februari 7, 2023 |
Diwani wa Kibosho Kati Bahati Mamboma |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi DC Moris Makoi. |
0 Comments:
Post a Comment