Mwenyekiti wa
CCM Wilaya ya Mwanga Mwl. Ibrahim Mnzava akimkabidhi
mwanachama mpya kadi ya kielektroniki kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 46 ya
kuzaliwa kwa chama hicho, katika Ofisi ya Kata ya Lang’ata,Mwanga. (Picha na
Kija Elias)
Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mwanga, kimeandikisha wanachama wapya 124 hafla ambayo imeenda sambamba na upandaji wa miti 50 kwenye kituocha Afya Lang’ata.
Hayo yanajiri ikiwa ni maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM ambayo kila kata, wilaya mkoani hapa zimeadhimisha kwa kufanya shughuli mbalimbali katika maeneoyao huku ikitarajiwa kimkoa kufanyika wilayani Same.
kimesema maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM ni kielelezo cha umoja wa kitaifa uliokengwa kwa misingi ya Amani, mshikamano na utulivu uliopo hapanchini Tanzania.
Akizungumza katikamaadhimisho hayo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mwanga Mwl. Ibrahim Mnzava, alisema ni jukumu la kila mwanachama kuzielekeza katika kukiimarisha na kukijenga chama kwani mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 46 ya CCM ni mengi.
Kwa upande wake Kaimu
Katibu wa CCM Wilaya ya Mwanga Paulo Bina, amesema katika maadhimisho hayo
wamefanikiwa kupanda miti 50 kwenye kituo cha afya Lang'ata,
kuingiza wanachama wapya 124 pamoja na kuwapatia kadi mpya za kieletroniki
wanachama 74.
0 Comments:
Post a Comment