Tuesday, February 21, 2023

Afisa Tarafa Moshi Magharibi kikwazo upanuzi wa barabara ya Mwembeni

Miti inayozuia utoaji wa kibali cha upanuzi wa barabaraya Longuo B,Moshi 

IMEELEZWA Afisa Tarafa Moshi Magharibi, Moshi mkoani hapa ni kikwazo cha upanuzi wa barabara baada ya kudaiwa kuomba rushwa ya miti ili kitolewe kibali cha ukataji wa miti hiyo kupisha ujenzi wa barabara.

Hayo yanajiri wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Moshi kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho huku jina laAfisa Tarafahuyo anayefahamika kwa jina la Senzia Masafiri Lushino likitajwa kuwa kikwazo cha ujenzi huo.

Akichangia hoja ya upanuzi wa barabara ya Longuo B,Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Jonathan Mabhiya alisema kumekuwa na vikwazo kutoka wilayani kuhusu utekelezaji wa upanuzi wa barabara hiyo.

“Niliwahi kutembelea Kata ya Longuo B kuna ufunguzi wa barabara mpya, wananchi wako tayari kutoa baadhi ya miti yao ikatwe barabara iweze kufunguliwa ili Tarura waanzematengenezo na Tarura wako tayari, lakini tatizo ni kikwazo kikubwa ni viongozi kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya,” alisema Mabhiya.

Aidha Mabhiya aliweka bayana kuwa muhtasari wa upanuzi wa barabara hiyo umefungiwa katika makabati ya wilayani tangu mwaka 2017 bila utekelezaji wowote hali inayotia ugumu kutekeleza mipango ya chama iliyojiwekea ifikapo 2025.

“Waliandika mhutasari uko ofisini kwako toka mwaka 2017 lakini tatizo ni kibali ambacho kimekuwa kikwazo kupatikana,” aliongeza Mabhiya.

Hata hivyo Mabhiya aliiomba ofisi ya mkuu wa Wilaya kushughulikia changamoto hiyo hasa ikizingatiwa Afisa Tarafa wa Longuo B amekuwa akinyoshewa kidole cha lawama kwa kutaka rushwa ya miti ili achane mbao kwa ajili ya kupanulia nyumba yake.

“Tunaiomba ofisi ya mkuu wa wilaya suala hili la barabara ya Longuo ambayo taarifa ilisha letwaofisini kwako ulifanyie kazi kibali cha uvunaji miti kiweze kupatikana ili barabara hiyo iweze kuanza kutengenezwa na wananchi kutoa eneo lao huko mkoa wa Kilimanjaro hata hatua moja tu barabara iweze kutanuliwa ni shida sasa hawa waliokubali kutoa eneo lao kwa ajili ya kipisha barabara tena bila kuomba fidia,” alisisitiza.

Kwa upande wao mkazi wa Longuo B aliyejitambulisha kwa jina la Ephraim Shao alisema, “Mimi nilikuwa shahidi namba moja katika kufuatilia kupata kibali cha kuvuna miti ili kupisha ujenzi wa barabara, tunahitaji maendeleo  ili kupisha barabara.”

Pia Damas Shao alisema kuna wakati Afisa Tarafa huyoalikuja na kumtaka ampe miti baadhi ili aweze kuto kibali cha uvunaji wa miti kwa ajili ya upanuzi wa barabara

"Mimi ndio mmiliki wa eneo  hili na kukawa na masharti ya kutoa rushwa ya miti kumi bure ana ujenzi wa nyumba yake kutoka kwa afisa tarafa ili aweze kunipa kibali cha kuvuna miti yangu na mimi nilishaapa siwezi nikatoa rushwa hadi sasa sijatoa chochote," alisema Mzee Shao.

Diwani Benedict Mwashamba alisema“wakati nikiingia kama Diwani wa Longuo B Tulikuwa na malengo ya kupata huduma bora na changamoto kubwa eneo letu lilikuwa halina maeneo kabisa ilikuwa barabara tulikaa na wananchi ili kujadili na tukaandika muhtasari na kuipeleka; watendaji wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya hasa huyu Afisa Tarafa ambaye alianza kutengeneza malalamiko,wananchi hakuna aliyepeleka malalamiko,”

Mwashamba aliongeza kwa sasa kinachotakiwa ni kutolewa kwa kibali cha uvunaji wa miti ili upanuzi wa barabara ufanyike kwa maendeleo ya wananchi wenyewe.

Mkuu wa Wilaya wa Moshi Kishare Makori alisema ameshangazwa na watendaji wa ofisi yake kushindwa kutoa kibali huku wananchi wakiwa tayari kutoa maeneo yao kwa ajili ya maendeleo yao, na aliagiza kuletewa nyaraka zote (muhtasari) wa suala hilolaupanuzi wa barabara ili aweze kutoa kibali hicho.





Mzee Damas Shao anayedai kuomba rushwa ya miti na Afisa Tarafa wa Moshi Mgharibi ili kupewa kibali cha uvunaji miti kupisha ujenzi wa barabara ya Mwembeni mtaa wa Kitandu, Longuo B


0 Comments:

Post a Comment