Sunday, March 1, 2020

Haji Manara abebwa mbio za Tigo Kili Half Marathon 2020

Haji Manara akimaliza kilometa 21 ya Tigo Half Marathon 2020 
Ujio wa Msemaji wa Simba Haji Manara umekuwa chachu ya mbio hizo kufanikiwa kwa kiasi kikubwa, uwingi wa mashabiki na wapenzi wa riadha umeongezeka baada ya kusikia ujio wake na kila mmoja alitaka kupiga naye picha kuonyesha kumuunga mkono katika mbio hizo. 

Vituko kwake haviishi ndio siri ya umati kutaka kujua atawaachia kumbukumbu gani katika mbio za mwaka huu, hakika amefanikiwa kufanya hivyo akitumia saa 1:53:20 katika kilometa 21 hata kama kipande kama cha kilometa mbili hivi cha mbio hizo akionekana kubebwa na bodaboda.




0 Comments:

Post a Comment