Julian Assange ni muasisi wa mtandao wa
WikiLeaks aliyesimamia uchapishwaji wa nyaraka kadhaa za siri kutoka serikali
kadhaa duniani.
Mei 2019 serikali ya Marekani ilimfungulia muasisi huyo wa
tovuti ya uvujishaji wa nyaraka za siri Wikileaks mashitaka ya kuvunja Sheria
za Upelelezi kwa kuchapisha nyaraka za kijeshi na kidiplomasia mnamo mwaka wa
2010.
Wizara hiyo iliorodhesha mashitaka 17 mapya dhidi ya Assange, ikimtuhumu
kwa kumuagiza na kumsaidia mtalaamu wa ujasusi, Chelsea Manning, kuiba nyaraka
za siri za Marekani, na pia kwa njia ya kiholela kuviweka hatarini vyanzo vya
siri katika Mashariki ya Kati na China ambavyo vilitajwa kwenye nyaraka hizo.
Alizaliwa Julai 3,1971 mjini Townsville nchini
Australia. Akiwa na umri wa miaka sita wazazi wake walitengana akawa anatanga
tanga na mamake. Hadi akiwa na miaka 16 waliishi miji 50 na kuhudhuria shule
37. Haya si maisha ya kawaida.
Mwaka 1987 akiwa na miaka 16 alianza
kujihusisha na shughuli ya kuharibu mitandao- inayoitwa kwa kimombo “hacking”.
Alitiwa nguvuni na wenzake mwaka 1991- na kesi iligharimu dola laki moja.
Hakimu alisema angehukumiwa jela miaka 10 kama asingekuwa na maisha ya
kuhamahama na ghasia utotoni.
0 Comments:
Post a Comment