WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika uzinduzi wa uboreshaji wa daftari la wapiga kura, utakaofanyika
mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro Julai 18 mwaka huu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge na Watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama
ameyasema hayo mwishoni mwa juma wakati alipotembelea eneo litakapofanyikia
zoezi la uzinduzi katika uwanja wa Mandela, ulioko eneo la Bomambuzi, Manispaa
ya Moshi.
Amesema uboreshaji wa daftari hilo utaanzia katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ambapo kwa mkoa wa Kilimanjaro ndipo kutakapofanyika uzinduzi huo.
Waziri Mhagama amesema kuwa utaratibu huo ni wa kawaida ambao sheria inataka Tume ya uchaguzi kama sehemu ya majukumu yake ya kuboresha daftari la wapiga kura.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya uchaguzi NEC, Jaji Semistacles Kaijage, alisema zoezi hilo linalotarajiwa kuzinduliwa Julai 18, mwaka huu, litawahusu wale ambao hawakupata nafasi ya kujiandikisha hapo awali.

0 Comments:
Post a Comment