Maelfu wa Watunisia na
viongozi wa mataifa mbalimbali wamejitokeza leo kuuaga mwili wa aliyekuwa rais
wa kwanza aliyechaguliwa kwa njia za kidemokrasia, Beji Caid Essebsi ambae
amefariki akiwa na umri wa miaka 92, akiliacha taifa hilo la Afrika ya
Kaskazini likikabiliwa na wasiwasi mpya wa kisiasa.
Maelfu ya raia walijipanga
barabarani kutoa heshima zao za mwisho, wakati mwili wa marehemu ulipokuwa
ukipitishwa huku wakisema "Maisha Marefu Tunisia" na kupeperusha
bendera ya taifa lao yenye rangi nyekundu na nyeupe.
Mfalme wa Uhispania, rais
wa Ufaransa na Mfalme wa Qatar Tamim bin Hamad Al-Thani na rais wa mpito wa
Algeria Abdelkader Bensalah walihudhuria ibada ya mazishi iliyofanyika katika
makazi ya rais mjini Tunis.
Usalama uliimarishwa vikali baada ya kuwepo kwa
kitisho cha ugaidi chenye kuhusishwa na kundi la Dola la Kiislamu.
Rais Essebsi
ambae atazikiwa umbali wa kilometa 7 kutoka katika makazi ya rais, alichaguliwa
kuiongoza Tunisia Desemba 2014 kukikamilisha kidemokrasia ya kipindi cha mpito
katika nchi hiyo baada ya vuguvugu la mapinduzi ya wananchi mwaka 2011
lililomuondowa madarakani mtawala wa kiimla Zine Ebadine Ben Ali aliyeitawala
nchi hiyo kwa muda mrefu.
CHANZO: DW
0 Comments:
Post a Comment