Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa ameagiza vijana
wote waliohusika katika ujenzi wa reli ya kutoka Dar es Salaam, Tanga hadi
Moshi ambao kwa sasa ni vibarua wanapaswa kubadilishwa na kuwa watumishi wa
kudumu wa shirika la Reli Tanzania
(TRC).
Akizungumza wakati akilipokea treni la kwanza mjini
Moshi, baada ya kutoonekana kwa miaka 17 Waziri Mkuu Majaliwa alisema
“Hawa waliofanya kazi hii , ambao ni vibarua sasa
wanapaswa wabadilishwe wawe watumishi wa kudumu ili waweze kupata ajira za
kudumu kwenye eneo hili, nataka ajira
zao zikamilike kwa wakati ili waendelee kuitunza reli hii , wataikarabati, na
wao watakuwa sasa watumishi ambao watakaoendelea kuifanya reli hii iwe inafanya
kazi siku zote bila ya mtu yeyote kudokoa chuma.”
Aidha Waziri Mkuu Majaliwa alisema kukamilika kwa reli
hiyo kutaongeza ufanisi wa usafirishaji wa shehena ya mizigo, hivyo kuliongezea
shirika mapato zaidi.
“Jitihada hizi zinafanywa na serikali lengo likiwa ni
kufikisha huduma kwa wananchi wote wakiwamo wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro,”
alisisitiza Waziri Mkuu Majaliwa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwapungia mikono wananchi
waliyofika kushuhudia uzinduzi wa treni ya mizigo katika reli ya Kaskazini
uliyofanyika katika stesheni ya reli Moshi, Julai 20.2019. (PICHA ZOTE KWA
HISANI YA WAZO HURU BLOG)
|
Vibarua wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) waliongaziwa nuru na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kulipokea treni la mizigo mjini Moshi Julai 20, 2019. |
0 Comments:
Post a Comment