Jux |
Nandy |
Kinyang’anyiro cha kumpata Mlimbwende wa Mkoa
wa Kilimanjaro mwaka huu (Miss Kilimanjaro 2019) yanatarajiwa kufanyika hii leo
mjini Moshi.
Wasanii watakaopamba kinyang'anyiro hicho kitakachofanyika Kili Home ni Jux na Nandy.
Akizungumza na Tanzania Daima Mkurugenzi wa
taasisi Dees Bridal & Entertainment Dotto Olafsen alisema maandalizi ya mashindano
hayo yamekamilika kilichobaki ni warembo waonyeshe uwezo wao katika jukwaa
kuwania nafasi ya tatu za juu kuwakilisha mkoa katika michuano ya kanda.
“ Kinyang’anyiro hiki kitafanyika Kili Home
hapa mjini Moshi, ninaamini mashindano ya safari hii yatafana sana kwani
tumewapika vya kutosha kilichobaki ni wao wenyewe kuwania taji la mwaka huu,”
alisema Olafsen.
Hata hivyo Olafsen alitaja viingilio vya
kinyang’anyiro hicho VIP A itakuwa Shilingi 200,000/=, VIP B itakuwa Shilingi 40,000/=
na Kawaida itakuwa ni Shilingi 10,000/=.
Walimbwende hao ambao wametoka katika fani
mbalimbali ikiwamo walimu, wafanyabiashara, madaktari na wanafunzi wa vyuo
vikuu watachukua vikali kuwania taji hilo.
Walimbwende hao walizuru Shule ya Sekondari ya
Machame Girls ikiwa ni sehemu ya kutoa hamasa kwa wanafunzi kujitambua na
wajibu wanaotakiwa kuutenda.
Mbali na hilo walimbwende hao walipata
kuhudhuria Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo Manispaa ya Moshi iliadhimisha Juni
15 mwaka huu katika shule ya sekondari ya Majengo ili kuhamasisha jamii kuhusu
malezi ya watoto ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili.
“Katika kampeni yetu hiyo ya kuzuia mimba za
utotoni tumegundua kuwa, baadhi ya watoto tayari wameshaathiriwa na tatizo hilo
na kuachishwa masomo kwani serikali hairuhusu mwanafunzi aliyezaa kuendelea na
masomo, ” alisema Olafsen.
Olafsen aliongeza kuwa kambi ya walimbwende
hao imedumu kwa takribani miezi miwili ambapo katika kambi hiyo walikuwa
wakifanya mazoezi na kufanya shughuli za kijamii.
STORY BY: Jabir Johnson
0 Comments:
Post a Comment