Thursday, July 4, 2019

MAKTABA YA JAIZMELA: Julai 4, 1776 Uhuru wa Marekani






Leo ni miaka 243 (Julai 4, 2019) tangu Marekani ipate uhuru wake. Taifa la Marekani lilipata uhuru wake Julai 4, 1776. 

Mwaka huo majimbo ya Marekani yalijikomboa kutoka kwa makucha ya Waingereza na baadaye kwa miaka tofauti yaliungana na kutengeneza taifa moja. Wamarekani wanakumbuka kumalizika vita vya mapinduzi lakini pia kukumbuka juhudi za kidemokrasia ilizopiga miaka 200 iliyopita. 

Vita vya Uhuru wa Marekani vilipigwa kati ya Uingereza na walowezi wa makoloni yake 13 kwenye pwani ya Amerika ya Kaskazini katika miaka 1775 hadi 1783. Jeshi la walowezi lililoongozwa na George Washington na wengineo lilishinda jeshi la Dola la Uingereza kwa msaada wa Ufaransa. 


Hivyo hatimaye makoloni hayo yakapata uhuru kama “Muungano wa Madola ya Amerika" au Marekani. Vita kamili vilisambaa. Mwanzoni Waingereza walikuwa na silaha na wanajeshi wengi zaidi, wakasonga mbele, lakini wanamgambo wa walowezi wakioongozwa na George Washington waliendelea kuwashambulia. 


Julai 4, 1776 wawakilishi kutoka makoloni yote walitangaza uhuru wa Muungano wa Madola ya Amerika. Bado Waingereza walisonga mbele wakatwaa pia mji wa New York. 


Lakini tangu mwaka 1777 Ufaransa ilianza kwa siri kutuma silaha kwa Wamarekani; mwaka 1778 Ufaransa, Hispania na Uholanzi ziliungana na kutangaza vita dhidi ya Uingereza. Manowari za Ufaransa zilishambulia meli za Waingereza zilizopeleka silaha na askari kwenda Marekani. 


Mwaka 1781 sehemu kubwa ya jeshi la Uingereza lilishindwa kwenye mji wa Yorktown likalazimika kujisalimisha. Tangu siku hiyo mapigano yalipungua na mwaka 1783 Uingereza ikakubali uhuru wa makoloni yake ya awali. Wakazi wengi wa makoloni walioendelea kusimama upande wa Uingereza walihamia Kanada iliyobaki kuwa koloni. 


Jamii kubwa nchini Marekani ni wazungu, waafrika, waspaniola, waasia na wakimbizi kutoka nchi zilizovamiwa na Marekani kivita. Wenye asili ya Marekani wahindi wekundu mfano kama kabila la Cherokee wamemezwa. Huwezi kuzungumza uhuru wa Marekani bila kumtaja George Washington.


Kutokana na umuhimu wa Washington katika siasa za Marekani ikumbukwe kuwa yeye ndio mwanzilishi wa wazo la kuunda taifa lenye mfumo wa shirikisho na yeye ndiye alipendekeza kuunganishwa makoloni 13 ya awali na liundwe taifa moja mara baada ya kumalizika kwa vita ya ukombozi mwaka 1788 niyeye aliyependekeza jina linalotumika sasa la “umoja wa mataifa ya marekani” (United State of America) na niyeye aliyependekeza wazo la mfumo wa kuwapata viongozi wao wa taifa hilo mfumo ujulikanao kama “Mfumo wa Chaguzi kwa kongamano” ( Electro College).

Ikumbukwe George Washington aliongoza kikosi cha wanamgambo kwenye vita ya ukombozi na baadae kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa balaza la kuunda katiba (Constitution Convetion) huko Philadephia kwenye kongamano la katiba na yeye ndie muasisi wa utaratibu wa kupokezana vijiti katika utawala nchini marekani. 

Moja ya taratibu alizozipendekeza ndizo zinazoendelea kutumika nchini marekani mpaka leo na kuifanya katiba ya marekeni kuwa moja ya katiba bora dunia hadi sasa.

George Washington alizaliwa Februari 22, 1732 hadi Desemba 14, 1799 alipofariki dunia nyumbani kwake huko Mount Vernon Virginia alikuwa mwanasiasa, kiongozi wa kijeshi na rais wa kwanza wa Marekani kati ya 1789 na 1797 washington pia hutambulika kama baba wa taifa wa marekani pia ni miongoni mwa wasisi wa taifa hilo kati ya wasisi 22 wanaotajwa kwenye Agano la uhuru (independence Declaration) katika taifa hilo kubwa kiuchumi na linalotajwa kukomaa kisiasa.

Washington alizaliwa kama mtoto wa pili wa mlowezi Augustine Washington katika koloni ya Virginia iliyokuwa mali ya mfalme wa Uingereza (lakini alikuwa ni mtoto wa kwanza wa Augustine Washington kwa mama yake Mary Ball Washington ambaye alikuwa ni mke wa pili wa Augustine Washington ).

Wazazi walikuwa na mashamba makubwa ya tumbaku lilolimwa na watumwa Waafrika. George alisoma shule miaka michache hakuendelea sana kielimu. Baada ya shule alianza kazi ya upimaji wa ramani (surveyor).


Baada ya kifo cha kaka yake mdogo alirithi shamba kubwa lilokuwa mali ya kaka yake pamoja na watumwa akawa mkulima tajiri huko Virginia. 

Sehemu ya urithi ilikuwa cheo cha msimazi wa wanamgambo pia waliokuwa kikosi cha kijeshi cha hiari waliotakiwa kusaidiana na wanajeshi wa Waingereza kutetea koloni dhidi ya majirani Waindio (red indies) na Wafaransa katika vita ya (French Indian War) walioenea katika maeneo ya kusini kutoka koloni yao ya Kanada - Quebec.

1 comment:

  1. Hey guys! If you want Affordable Assignment Writing help then go with a quality writing content company. Quick Assignment is offering writing services for research papers, dissertation, case study, essay writing etc. at reasonable cost.

    ReplyDelete