Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage. |
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewaonya wote
watakaokiuka kanuni katika Uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kuwa watachukuliwa hatua za kisheria kwani
zoezi hilo linaendeshwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Akizungumza katika mkutano wake na wanahabari katika
ukumbi mdogo wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, juu ya ujio wa Waziri
Mkuu katika uzinduzi wa Uboreshaji wa Daftari hilo utaofanyika katika viwanja
vya Mandela, Manispaa ya Moshi Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage
alisema hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale wataobainika kulaghai au
kuwasilisha taarifa za uongo ikiwamo mtu kujisajili mara mbili huku akijua kuwa
atakuwa na vitambulisho viwili.
Jaji Kaijage alisema alisema kuwa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi tayari imemaliza mandalizi yake ya Uboreshaji wa Daftari kwa mujibu wa Sheria, Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa , ambapo atazindua zoezi hilo ambalo litaanzia katika mikoa ya
Kilimanjaro na Arusha na baadae litaendelea katika mikoa mingine kwa mujibu wa
ratiba.
Alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa jukumu la kikatiba la kusimamia na
kuratibu uandikishwaji wa Wapiga kura
katika uchaguzi wa Rais na wabunge
kwa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bara nah ii ni kwa mujibu wa cIbara
ya 74(6) na( D) ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
utafanyika katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa vipindi tofauti
kulingana na mgawanyo wa mikoa kikanda kwa mujibu wa ratiba itakayotolewa na
Tume hiyo.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi hufanya uboreshaji wa Daftari
la Kudumu la Wapiga Kura kwa mujibu wa Ibara ya 74 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inayoipa Tume mamlaka ya kusimamia na kuratibu
uandikishaji wa Wapiga Kura katika Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya
Muungano pamoja na Madiwani kwa Tanzania Bara.
0 Comments:
Post a Comment