Rais Nicolas Maduro yupo katika mbinyo na shinikizo kubwa kutoka mataifa ya magharibi na washirika wake; yakimtaka kuachia kiti hicho. |
Umoja wa Ulaya unajitayarisha kuweka vikwazo zaidi dhidi
ya Venezuela vikiwalenga maafisa ambao wanashutumiwa kuhusika na mateso na
ukiukaji mwingine wa haki za binadamu.
Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Federica
Mogherini amesema katika taarifa leo kuwa Umoja huo unafanyakazi pamoja na
Umoja wa Mataifa kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinaheshimiwa nchini
Venezuela kufuatia ripoti za ukiukaji unaofanywa na majeshi ya usalama.
Mogherini amesema kuwa Umoja wa Ulaya uko tayari
kufanyakazi kuelekea kuweka vikwazo vya malengo maalum kwa wanajeshi mmoja
mmoja wa majeshi ya usalama waliohusika na utesaji pamoja na ukiukaji mwingine
mkubwa wa haki za binadamu.
Umoja wa Ulaya umeiwekea vikwazo Venezuela tangu mwaka
2017, ikiwa ni pamoja na vya silaha pamoja na vifaa vinavyotumika kufanya
utesaji.
0 Comments:
Post a Comment