Leo ni siku ya vipapatio vya kuku. Kila Julai 29 kila
mwaka ni maalum kwa ajili ya Vipapatio vya Kuku.
Imeelezwa na wataalamu wa
masuala ya lishe kuwa kwa mwaka tunakula vipapatio 290.
Hakika ni miongoni mwa
viungo vitamu ambavyo huliwa na wengi. Nchini Marekani vimekuwa vikifahamika
kama Buffalo Wings. Kipapatio cha kuku kimegawanyika sehemu kuu tatu “wingette,
drumette na tip.”
Utamaduni wa vipapatio vya kuku nchini Tanzania umekuwa
tofauti kutokana na eneo. Watu wa pwani hufurahia sana ulaji wa vipapatio.
Lakini maeneo mengi ya bara vipapatio hupewa watoto na mgeni wa heshima huwezi
kumwekea nyama hiyo. Kwa ufupi sikukuu hii ilianza kuadhimishwa mwaka 1977
katika mji wa Buffalo jijini New York nchini Marekani.
Mkoani Kilimanjaro na kanda ya kaskazini kwa
mara ya kwanza siku hii ilisikika katika vyombo vya habari Jumatatu ya Julai 29, 2019 katika kituo
cha Redio Kili FM mjini Moshi katika kipindi cha Kili Breakfast (saa 12:30 hadi
4:00 asubuhi) kupitia mtangazaji wa kipindi hicho Johnson Jabir ambaye
aliendesha mjadala kuhusu vipapatio vya kuku.
Je unafahamu namna ya kuandaa
vipapatio vya kuku hadi kuwa mlo kamili.
MAHITAJI
Vipapatio hivi vya kuku unaweza kuvipika na kula kama
kitafunwa wakati wa kupumzika na familia au wakati wa vikao muhimu na marafiki.
·
Vipapatio vya kuku 10 (Unaweza kuwa na idadi
yeyote, kutegemea na walaji)
·
Vijiko 5 vya sauce ya pilipili (Unaweza pia
kuwa na pilipili ya kuongezea)
·
Siki iliyochujwa (distilled Vinegar)
·
Mafuta ya kukaangia (Vizuri kama ukiwa na
mafuta yanayotokana na mimea)
·
Vijiko 4 vya majarini (siagi au margarine)
·
Chumvi
·
Pilipili (hii ya kuongeza utamu)
·
Pilipili manga
Vitu vya ziada kwa kuku (si lazima)
·
Kitunguu saumu cha unga
·
Tangawizi
·
Limao
Tunatengeneza hiki chakula katika sehemu mbili tofauti -
tutakaanga kuku, wakati huo huo tutapika sauce yetu ya pilipili. Kumbuka vipapatio
vinapaswa viive vizuri hadi vikauke na kubadilika rangi. Inachukua kama dakika
10 hivi. Toa vipapatio vyako na weka kwenye tissue paper, ili wachuje mafuta
vizuri.
0 Comments:
Post a Comment