Monday, July 29, 2019

MAKTABA YA JAIZMELA: Benito Mussolini ni nani?



Benito Mussolini alikuwa mkuu wa serikali ya Italia kutoka mwaka 1922 hadi 1943. 

Huyu ndiye mwanzilishi wa Ufashisti na anachukuliwa na ulimwengu wa magharibi kuwa ni dikteta kutokana na namna alivyokuwa akiwaongoza raia wake katika taifa hilo la Italia.

Aliiongoza Italia katika vita tatu na ya mwisho alishindwa mbele ya watu wake. Musssolini alizaliwa Julai 29, 1883 na kufariki dunia Aprili 28, 1948.  Mussolini alizaliwa katika kitongoji cha Dovia di Predappio hapo hapo nchini Italia. 

Kwa hakika alizaliwa katika familia masikini mno ambayo ilikuwa ikiishi katika nyumba ya vyumba viwili tu. Baba yake alikuwa mfua vyuma na mfuasi wa falsafa ya ujamaa (mfumo wa maisha ambao ulikuwa ukiruhusu kushirikiana katika ardhi na vitu kwa usawa miongoni mwa jamii). 

Mama yake alikuwa mwalimu wa shule ya chekechekea. Licha ya kuwa na akili tangu utoto wake lakini Benito alikuwa ni mtu wa vurugu siku zote za maisha yake. Alikuwa mwanafunzi maskini hivyo hakuwa na muda mzuri wa kujifunza mambo mengi. Baadaye alifanikiwa kwenda katika shule ya bweni ya Faenza, Italia. 

Akiwa huko alifanya tukio la kuogofya pale alipomchoma kisu mwanafunzi mwenzake, hatimaye alifukuzwa shule. Baada ya kupata Astashahada yake mwaka 1901 aliingia katika kazi ya mama yake ya ualimu ambako yeye alifundisha sekondari. 

Mwaka 1902 alikwenda Uswisi ukiwa ni mpango wake wa kutoroka ili asiweze kwenda jeshini, akiwa huko alijiunga na wanaujamaa wengine. Alirudi Italia mwaka 1904 ambapo alitumia muda wake mwingi jeshini na katika siasa kikamilifu. 

Mussolini alikuwa mwanachama wa chama cha Kijamaa tangu mwaka 1900 na akiwa humo ndipo alipoanza kuwa na mvuto kwa wengi. Katika hotuba zake na makala zake alikuwa mkali na mwenye vurugu, mwenye kukosoa mapinduzi kwa gharama. Mussolini aliwahi kuwa mhariri wa gazeti la chama la kila siku la Avanti. Wakati huo akiwa na umri wa miaka 29. 

Kinachovutia kwa Mussolini ni kwamba alifanya mapinduzi katika muda mwafaka ambapo watu wa ardhi ile walikuwa wakiihitaji. 

Pia alikuwa akijua kuwa vita ya kwanza ya dunia itaizika Ulaya ya zamani na kuanza Ulaya isiyojulikana. Hivyo akaanzisha gazeti lake la Popolo d’Italia ambalo alilitumia kueneza falsafa yake ya Ufashisti.


0 Comments:

Post a Comment