Theresa May |
Julai 24, 2019 Boris Johnson aliyekuwa Waziri wa zamani wa mambo ya kigeni wa Uingereza alichaguliwa kuwa kiongozi wa chama tawala cha Conservatives nchini humo kuchukua nafasi ya Bi Theresa May.
Hii ilimaanisha Boris Johnson sasa atakuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza baada ya May kutangaza kujiuzulu mwezi uliyopita.Boris aliye na miaka 55 alimshinda mpinzani wake Jeremy Hunt kwa wingi wa kura katika uchaguzi huo.
Boris Johnson anatazamiwa kuapishwa rasmi kama Waziri
Mkuu wa Uingereza. Johnson pia anatarajiwa kutangaza majina ya kundi
atakalolipa majukumu ya kuendesha mchakato wa kuiondoa Uingereza katika Umoja
wa Ulaya.
Boris Johnson ataanza kuiongoza Uingereza kuanzia hii leo mchana
wakati Waziri Mkuu Theresa May atakapomkabidhi rasmi mkoba huo wa uongozi. May
alitangaza kujiuzulu mwezi uliyopita baada ya kushindwa kuwashawishi wabunge
kuunga mkono mapendekezo yake ya kuiondoa nchi hiyo katika Umoja wa Ulaya.
Boris
anaingia katika ofisi ya Downing Street wakati Uingereza ikiwa imegawika juu ya
suala la Brexit na kudhoofika kutokana na mgogoro huo wa kisiasa wa miaka
mitatu tangu kura ya maoni ya kujiondoa katika Umoja huo ilipopigwa.
Boris Johnson |
0 Comments:
Post a Comment