Wajumbe wa Tume maalum iliyoundwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kufuatilia madeni katika vyama vya ushirika Tanzania wakiwa mkoani Kilimanjaro Julai 30, 2019. |
Chama
Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro KNCU (1984) Limited, kimefanikiwa
kukirejesha mikononi mwa serikali kiwanda cha kukoboa mpunga cha Kilimanjaro
Paddy Huling Company Limited (KPHC) ambacho Chama hicho kilikabidhiwa na serikali kwa mkataba wa ukodishaji tangu mwaka 1991.
Hayo
yamebainishwa na Mwenyekiti wa KNCU Prof. John Boshe kwenye Mkutano Mkuu wa 35
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Coffee Tree Hotel uliopo mjini Moshi mkoani hapa.
Prof.
Boshe alisema kuwa kabla ya kukikabidhi kiwanda hicho KNCU walifanya tathmini
ya hali ya kiwanda hicho na kuonekana kwamba kiwanda hicho hakitakuwa na tija
tena kwa Chama hicho kwani kimeendelea
kuwa mzigo kwa Union.
“Ndugu
wajumbe wa mkutano Mkuu , tulipokea barua ya serikali yenye kumb. Namba
CKB.85/366/01/57 ya Julai 2018 ambayo ilikuwa ikituelekeza kwamba tunatakiwa
kukabidhi kiwanda hiki cha kukobolea mpunga kilichopo Chekereni,”alisema Prof.
Boshe.
Alisema
KNCU ilikabidhiwa na serikali kiwanda hicho cha kukobolea mpunga mwaka 1991
lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza kiwanda hicho hakikuweza tena
kuendelea kufanya kazi jambo ambalo limeendela kuwa mzigo kwa KNCU kwa
kuendelea kulimbikiza madeni yakiwemo ya kulipia pango la kodi ambayo ilikuwa
hailipi kwa muda mrefu ya kiasi cha shilingi 200,000 kwa kila mwezi.
Mkutano wa 35 wa KNCU Julai 30, 2019 |
STORY BY: Kija Elias, Moshi... Julai 30,2019; PHOTO BY: Joseph Tesha
0 Comments:
Post a Comment