Nelson Rolihlahla Mandela
alizaliwa Julai 18,1918 na alifariki Desemba 5, 2013. Huyu ni
rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia
nchini Afrika Kusini.
Alikuwa mwanasheria na mwanachama wa ANC aliyepinga siasa
ya ubaguzi wa rangi Apartheid katika Afrika Kusini. Mandela alitumikia kifungo
cha maisha kwa miaka 27 kutokana na harakati zake za kuupinga ubaguzi wa rangi.
Alifungwa
katika kisiwa cha Robben. Baada ya kuachiliwa huru mwaka 1990 alianzisha sera ya
maridhiano. Mwaka wa 1993, pamoja na Frederik Willem de Klerk alikuwa mshindi
wa Tuzo ya Nobel ya Amani.
0 Comments:
Post a Comment