Uongozi wa soko la kuu la Mitumba la Memorial (King George Memorial), katika manispaa ya Moshi umeahidi kushirikiana na dawati la jinsi katika jeshi la Polisi, kupiga marufuku wafanyabiashara wa soko hilo kwenda sokoni hapo na watoto chini ya miaka mitano.
Aidha kabla ya kufanyika kwa zoezi hilo,
uongozi huo utatoa elimu kwa wazazi na walezi wenye watoto kuanzia miaka sifuri hadi mitano ambao wanaonekana
sokoni hapo kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa moja usiku wakiwa na wazazi wao.
Mwenyekiti wa soko hilo, Godfrey Shayo, alisema hayo wakati wa utafiti wa kuongeza uelewa, uwajibikaji wa huduma bora za malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto (ECD), unatekelezwa na Muungano wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC) kwa kushirikiana na taasisi ya CiC ya Ireland.
“Ukija sokoni hapo majira ya saa 11 Alfajiri utaona wazazi na walezi wakiwa na watoto wachanga….huu ni ukatili na unaathiri afya ya mtoto na malezi yake ya baadaye, tumeliona hili na tunaandaa mpango wa kutoa elimu kabla ya kuchukua hatua”alisema.
Kwa upande wao wenyeviti wa masoko la Mbuyuni, Lameck Mziray na mwenyekiti mtaa wa soko la Pasua, Rahibu Juma walikiri kuwapo kwa changamoto inayoathiri afya za watoto hao lakini waliahidi kuandaa mpango wa ushirikishwai na wafanyabiashara ili kujadili suala hilo.
Daktari bingwa mwandamizi wa afya ya jamii, Uzazi na magonjwa ya akinamama, Dkt Moke Magoma alisema alisema malezi hayo yasipodhibitiwa yatachangia kwa asilimia kubwa kujenga taifa la kizazi kisicho na mwelekeo na chenye urahisi wa kujihusisha na matukio ya uhalifu.
Alisema maeneo ya ujasiariamali siyo salama kwa malezi na makuzi ya watoto kiafya na kisaikolojia na kwamba jambo la msingi ni kwa wazazi na walezi wakatafuta mbinu mbadala ili kuokoa kizazi hicho.
Nao baadhi ya wazazi Mwantumu Swalehe na Hadija Omary walidai wanalazimika kwenda katika maeneo ya ujasiriamali na watoto kutokana na kukosa imani na walezi wengine hususani ndugu wa karibu wa Kiume ambao huwafanyia ukatili wa kingono.
“Baba usituone tunahangaika na watotowetu huku sokoni, tunafahamu kwamba ni hatari kwa afya lakini inatulazimu kutokana na kubadilika kwa dunia ya sasa…huyo unayemwamini ndiye anaye kuharibia mtoto, serikali ilitizame hili”alisema Swalehe.
STORY BY: Nakajumo James, Moshi

0 Comments:
Post a Comment