Mahakama ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro imemhukumu kifungo cha miaka 12 jela au kulipa faini Lawrensia Massawe (56) baada ya kupatikana na hatia ya kughushi nyaraka za serikali kisha kujipatia kiasi cha shilingi milioni 13.5
Mshtakiwa ambaye alikuwa Afisa Elimu na Mratibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na Watoto (UNICEF), alitakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 1.2 na kurudisha kiasi cha fedha alichoghushi.
Aidha mahakama hiyo ilimwachia huru mhasibu wa Halmashauri ya wilaya hiyo Tumpala Ambakyse baada ya mahakama hiyo kumuona hana hatia.
Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama hiyo Jasmine Abdul, baada ya kuridhika na ushahidi wa watu 23 uliotolewa na jamhuri Mahakamani hapo usioacha shaka ndani yake,na mahakama alimtia hati mshtakiwa kwa makosa 12 ikiwamo ya kughushi na kujipatia fedha hizo.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa( TAKUKURU) Suzani Kimaro washitakia kuwa Oktoba 2017 w walifanya makosa mbali mbali ikiwamo ya alighushi nyaraka na kujipatia kiasi cha sh,13.5 kinyume na kifungu namba 28(1) cha sheria ya kupambana na kuzuia rushwa kifungu namba 11 cha 2007
Fedha hizi zilitolewa sh,23.9 milioni zilitolewa na UNICEF kwa ajili ya Halmashuri hiyo kwa ajili ya mafunzo na kwenda kuwaibua wanafunzi vijijini ambao hawakufanikiwa kupata elimu lakini sh,13.5 .zilipotea
“Mtuhumiwa aligushi nyaraka ambazo zilionyesha alitoa semini kwa siku mbili kwa wenyeviti wa vijiji 37, maafisa watendaji 36, watendaji wa kata 12 ,waratibu elimu kata 12, maafisa Tarafa 5 na kila mmoja alitakiwa kulipwa posho kiasi ya shilingi 180,000 lakini walilipwa sh, 45000 kitu ambacho aliidanganya Halmashauri” alieleza Kimaro
Kabla ya kutoalewa kwa hukumu hiyo mwendesha mashitakab aliomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali dhidi ya mshitakiwa kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo.
Hata hivyo Ester Kibanga ,wakili anayemtetea mshitakiwa aliomba mahakama hiyo kumpunguzia adhabu kwa sababu ,ni mgonjwa ana mume ana wajukuu wanaomtegemea pia ana miaka mingi
Ambapo hakimu wa mahakama hiyo alisema mahakama imezingatia utetezi huo na kumtaka kulipa faini ya shilingi milioni 1.2 au kwenda jela miaka 12 na pia mahakama hiyo ilimtaka kurejesha kiasi cha sh,13.5 alizochukua kuzirejesha katika Halmashauri ya Siha, ambapo alifanikiwa kulipa na kukwepa kifungo.
0 Comments:
Post a Comment