Tuesday, July 2, 2019

Je, unafahamu namna ya kuboresha kumbukumbu



Julai 2 kila mwaka huwa ni siku maalumu kwa ajili ya kukumbushana kuhusu kuboresha kumbukumbu ili kuondokana na usahaulifu. 

Binadamu aliumbwa na ubongo ambao una uwezo wa ajabu wa kukumbuka mambo. 

Aliumba ubongo uwe kama hazina ambayo ingeweza kutumiwa daima bila kupoteza kitu. Labda unaona kwamba unasahau mambo mengi yanayoingia akilini mwako. Ni kama huwezi kuyakumbuka. 

Unawezaje kuboresha kumbukumbu yako? Ni tatizo la kawaida kusahau majina ya watu.  Akili zetu huchochewa tukiwa na mazoea ya kupendezwa na watu na vilevile mambo yanayoendelea karibu nasi. Ndipo itakapokuwa rahisi kuwa na upendezi tunaposoma au kusikia jambo linalotufaidi daima. 

Unapokutana na mtu, utakumbukaje jina lake? Kwanza tafuta sababu nzuri inayokufanya ukumbuke jina lake; Wataalamu wa elimu wanasisitiza kwamba ni muhimu kupitia habari uliyosoma. Profesa mmoja wa chuo kikuu alifanya uchunguzi, akathibitisha kwamba ukitumia dakika moja kupitia haraka habari uliyosoma, utazidisha mara mbili uwezo wako wa kukumbuka mambo hayo. 

Basi, baada tu ya kumaliza kusoma habari fulani—au sehemu yake kuu—jikumbushe mambo makuu ili uyakaze akilini mwako. Fikiria jinsi unavyoweza kueleza kwa maneno yako mwenyewe mambo mapya ambayo umejifunza. Ukijikumbusha jambo punde tu baada ya kulisoma, utalikumbuka kwa muda mrefu. 

Kisha katika siku chache zijazo, tafuta nafasi za kujikumbusha mambo uliyosoma kwa kumweleza mwingine habari hiyo. Unaweza kumweleza mtu wa familia, mtu wa kutaniko, mfanyakazi mwenzako, mwanafunzi mwenzako, jirani, au mtu unayekutana naye katika huduma ya shambani.  

Tujihadhari tusiwe wasahaulifu. Tunapokabili changamoto za maisha.

0 Comments:

Post a Comment