Monday, July 22, 2019

KUTOKA WHATSAPP: Kutumbuliwa kwa January Makamba


January Makamba


Nusu saa baada ya kutangazwa kwa taarifa za kutumbuliwa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba, Waziri huyo aliyetumbuliwa amebandika katika akaunti zake za mtandaoni akisema;

“Kwa kweli nimeyapokea mabadiliko yaliyofanywa kwa moyo mweupe kabisa kabisa . Nitasema zaidi siku zijazo” kisha akaweka picha yake akiwa anacheka ameketi na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi.

Nionavyo mimi huu ni mwendelezo wa tabia na vitendo vya jeuri, dharau, kukosa nidhamu na kujifanya kujua kuliko wengine (much know) ambalo ni tatizo kubwa la January na watu wengine wenye tabia zake akina Nape Nnauye na wenzao ambao nahifadhi majina yao.

Kwa taaluma yangu ya kifalsafa, kwa haraka haraka katika post yake January Makamba anatuambia yafuatayo;

1. Kwamba japo ametumbuliwa, siku moja ataibuka na kuwa Rais wa Nchi kama ilivyokuwa kwa Mzee Mwinyi ambaye alijiuzulu Uwaziri wa Mambo ya Ndani kutokana na vifo vya Mahabusu kule Shinyanga na baadaye akaibuka kuwa Rais.
• Nataka kumwambia kijana mwenzangu January kuwa Mzee Mwinyi alijiuzulu lakini wewe umefukuzwa kwa kupanga njama za uhaini. Wewe umeondoka vibaya kwa kashfa mbaya sana kama kiongozi na ndani ya chama.
• Tena una bahati kwamba CCM ina utaratibu vinginevyo ingekuwa vyama vingine ungesikia umeshafutwa uanachama na Ubunge kupoteza. Hata hivyo hatujui ukifikishwa kwenye vikao vya chama itaamliwa nini. Yaani hayajaisha.

2. Kwamba kutumbuliwa kwako hakujakuuma ndio maana unacheka, umefurahia.
• Nataka nikwambie kuwa hili ni pigo kubwa sana kwako. Sikutabirii lakini usipojiangalia hapa ndio mwisho wa ndoto zako za kuukwaa Urais.
• Nataka nikwambie badala ya kufurahia unapaswa kutafakari mienendo yako kama inabeba matarajio yako? Au inayapoteza.
• Nataka kukwambia badala ya kufurahia unapaswa kujua kuwa dude hili linaweza kusababisha upoteze hata ubunge wako.
• Nataka kukwambia dude hili limeharibu heshima ya Baba yako katika Chama na Serikali. Dude hili sio la kufurahia hata kidogo.
• Nataka kukwambia sakata hili limesababisha upoteze wafuasi wengi ambao tulikuwa tunapendezwa na siasa zako, uongozi wako na ndoto zako. Limetuumiza sana. Sio la kufurahia hata kidogo.
• Nataka nikwambie huyo uliyekuwa ukimfanyia mikakati ya kumhujumu ni Mwenyekiti wa CCM atakayepitisha majina ya Wagombea ubunge 2020 na Serikali yake ndio itakayosimamia uchaguzi mkuu wa 2020.
• Nataka nikwambia huyo aliyekutumbua baada ya kung’amua mpango wako wa kumhujumu ndiye atakayepitisha majina ya wagombea Ubunge wa CCM 2025 na uchaguzi mkuu utafanyika mikononi mwake.
• Nataka nikwambia mahali pekee pa kutokukutana nae ni mwaka 2030 ambapo yeye atakuwa kwenye Baraza la Viongozi Wastaafu ambao wana karata yao ya kupata mgombea Urais.

3. Kwa kauli ya “Nitasema zaidi siku zijazo”
• Yawezekana unataka kujibu mapigo. UTAHARIBU.
• Yawezekana unataka kuomba radhi. MTIHANI.
• Yawezekana unataka kujitetea. UTAHARIBU.

4. Kwa kutumia picha ya Mzee Mwinyi.
• Hulingani nae na yeye alishaweka wazi kuwa anapongeza Mhe. Rais Magufuli na anamhusu. (Tazama video yake alisema hayo)

JIFUNZE
1. Kudhibiti mikono yako mitandaoni na maneno yako kinywani.
2. Kuamini kuwa wako wanaojua hata zaidi yako.
3. Kuheshimu Mamlaka na kuyatii na hasa unapokuwa katika nafasi za uongozi wa Mamlaka hiyo.
4. Utulivu wakati wa misukosuko. Usimuige Nape Nnauye na hurka zake. Mfano wa Mzee Mwinyi na Mhe. George Simbachawene unatueleza kuwa utulivu unalipa. Iga utulivu wa akina Mwigulu Nchemba na wengine wengi waliotumbuliwa. USIWASHWEWASHWE.
5. Ongea na Baba na mshauri atulie kwa sababu kuvuja kwa mazungumzo yenu kumeonesha kuwa lenu moja na hamna nia njema na Serikali hii.

Julius M.B
Mwana UVCCM
Kinondoni, DSM.

0 Comments:

Post a Comment