Alijulikana kama Princess Diana, lakini jina lake halisi ni "Diana Spencer", ambaye alichukuliwa na dunia kama mfano wa kuigwa kutokana na mapenzi yake kwa jamii hususani katika shughuli za kujitolea.
Princess Diana wa Wales, alizaliwa na Julai 1, 1961 akiwa ni mtoto wa nne katika familia ya John Spencer na Frances Roches iliyokuwa ikiheshimika na iliyokuwa na ukaribu na ukoo wa kifalme nchini Uingereza.
Katika utoto wake Diana alikulia katika maeneo yenye utulivu katika Estate ya Sandringham, na kusoma nchini humo pamoja na Switzerland.
Mwaka 1975 baba yake aliridhi taji la ufalme wa awali na kufahamika kama Earl Spencer na yeye kuanza kuitwa Lady Diana Spencer.
Maisha yake ya umaarufu yalianzia mwezi Februari mwaka 1981 alipotangazwa kuchumbiwa na mwana wa mfalme na mrithi mtarajiwa Prince Charles na kufunga ndoa yao iliyotangazwa dunia nzima Julai 29 mwaka huo huo.
Inasemekana kuwa, Ndoa ya wawili hao ilionyeshwa katika runinga za nchi hiyo na tukio hilo lilishuhudiwa na watazamaji zaidi ya milioni 750. Ndoa iliyofungwa katika kanisa la Mtakatifu Paul.
Wakati wa maisha yake baada ya ndoa Diana alijulikana kwa majina mengi likiwemo la Malkinia wa Wales, Duchess wa Cornwall na mengine mengi.
Diana aliendelea na maisha binafsi akiwa nje ya kasri ya kifalme na kuhusishwa na uhusiano wa kimapenzi na mtoto wa mfanyabiashara maarufu Dodi na mnamo Agosti 31, 1997 dunia ilipokea habari mbaya za kufariki dunia kwa kipenzi huyu wa jamii, kufuatia ajali ya gari mjini Paris, Ufaransa na mazishi yake kufanyika kwa heshima zote za kifalme na kuonyeshwa dunia nzima.
0 Comments:
Post a Comment