January Makamba |
Rais Dkt. John Magufuli amemteua George Boniface Simbachawene
kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
Simbachawene anachukua nafasi ya January Yusuf Makamba ambaye
uteuzi wake umetenguliwa. Wakati huohuo, Rais Magufuli amemteua Hussein Mohamed
Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.
Bashe anachukua nafasi ya Innocent Lugha
Bashungwa ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Biashara na Uwekezaji.
Katika hatua
nyingine, Rais Magufuli amemteua Balozi Dkt. Martin Lumbanga kuwa Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA). Dkt.
Lumbanga ameteuliwa kushika nafasi hiyo kwa kipindi
cha pili.
Uteuzi wa viongozi hao umeanza Julai 21, 2019.
ALICHOSEMA JANUARY MAKAMBA BAADA YA KUTIMULIWA
Kupitia Ukurasa wake wa Twitter, Makamba kaweka picha yake akiwa na mzee Mwinyi na kuandika; "Kwa kweli nimeyapokea mabadiliko yaliyofanywa kwa moyo mweupe kabisa kabisa 😊. Nitasema zaidi siku zijazo. "

0 Comments:
Post a Comment