Bondia wa Super Welter Weight
Mtanzania Hassan Mwakinyo Machi 21, 2020 anashuka ulingoni nchini Ujerumani
kupigana na bondia Mjerumani Jack Culcay kuwania mkanda wa ubingwa wa WBO
International Super Welter Weight.
Mwakinyo, 24, ambaye katika uzito wa Super Welter anashika
nafasi ya kwanza kwa ubora barani Afrika na namba 20 Duniani, atakuwa ni bondia
wa kwanza Mtanzania kugombea mkanda huo ambao ni wa pili kwa ukubwa baada ya
ule wa Dunia wa WBO uliokuwa unaishikiliwa na bondia Manny Pacquiao.
Mpinzani wake Jack Culcay ni bondia namba 1 kwa ubora Ujerumani
kwenye uzito wa Super Welter akishika nafasi ya 4 barani ulaya. Hassan Mwakinyo
akifanikiwa kushinda mkanda huu na kuutetea mara mbili atakuwa amejiweka katika
nafasi ya kugombea mkanda wa Dunia.
Mwakinyo anakwenda kupigana
pambano hili akiwa na rekodi nzuri ya Kushinda mapambano yake mawili ya mwisho
nje ya nchi moja dhidi ya Muingereza Sam Eggington na jingine dhidi ya
Muargentina Raul Ginzalenz rekodi inayombeba dhidi ya mpinzani wake.
0 Comments:
Post a Comment