Monday, March 23, 2020

RCL 2020: Babati Shooting Star ya Manyara

Ligi ya Mabingwa mikoa (RCL) ni miongoni mwa mashindano ya soka yanayosimamiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). 

Kutokana na janga la dunia la virusi vya Covid-19 mashindano mbalimbali yanayosimamiwa na TFF yamesimama kwa agizo kutoka serikalini ili kuepusha maambukizi zaidi ya virusi hivyo. 

Hata hivyo kwa mechi chache zilizochezwa tunakuleteza timu moja moja katika Kundi B ambalo lilipangiwa kuchezwa katika Uwanja wa Ushirika, mjini Moshi, Kilimanjaro. 

Timu zilizokuwepo kwenye kundi hilo ni Cable SC (Arusha), Muheza United (Tanga), Mbuyuni Market (Kilimanjaro), Nyamongo FC (Mara), Mweta FC (Mwanza), Huduma (Dar es Salaam) na Babati Shooting Star (Manyara).

Mashindano hayo yalianza Machi 14, 2020 lakini yalisimamishwa Machi 17, 2020 ikiwa ni mitanange sita tu iliyochezwa kutokana na kitisho hicho cha Covid-19.

TFF ilitoa taarifa yake kuwa mashindano yake yatasiamama kwa siku 30 kupisha wasiwasi uliopo na kwamba baada ya siku hizo kuna uwezekano mkubwa wa timu kutocheza na mashabiki.

Ifuatayo ni timu ya Babati Shooting Star FC katika PICHA.

Babati Shooting Star Lineup
Hassan Ukio, Haroun Hassan, Abdullah Banda, Nelson Haule, Steven Lusinde, Said Moyo, Yazid Iddy Mwenda, Emmanuel Anderson, Hassan Joseph, Gipron Marco, Dickson Mwakalinga.


Wa Akiba; Said Ndatu, Mazuu Simba, Swaleh Amiry, Ozil Mustapha, Ashraf Ally, Juma s. Moto, Juma Twalib.


STORY & PHOTO BY: Jabir Johnson
EMAIL: jabirjohnson2020@gmail.com
DATE: Machi 23, 2020




Abdullah Banda akipiga mkwaju wa adhabu ndogo nje kidogo ya lango la Cable SC.










0 Comments:

Post a Comment