Machi 12, 2005 mfanyabiashara wa Kimarekani Malcom Glazer alichukua mikoba
ya umiliki wa klabu ya Manchester United.
Familia hiyo ya Glazer ilianza kumiliki klabuu hiyo ya ligi kuu nchini
England hadi leo. Familia hiyo ndio wamiliki wa klabu nyingine ya American
Football ya Tampa Bay Buccaneers.
Glazer walianza kuingia taratibu katika umiliki wa klabu hiyo mnamo Machi
2003 walipochukua hisa ya asilimia 2.9 ambayo kwa wakati huo waliweka kiasi cha
pauni milioni tisa.
Taratibu waliendelea kuongeza hisa
ambapo Oktoba 2004 walikuwa wamefikia asilimia 30 ya hisa klabuni hapo
ambayo iliwaruhusu kuomba kuwa wamiliki.
Wanahisa wengine wawili JP McManus
na John Magnier walikuwa na asilimia 28.7 walijikuta wakishindwa
kuelewana na kocha Sir Alex Ferguson hivyo iliwapa wakati mgumu wa kuungana
kuchukua umiliki huo.
Mnamo mwaka 2005 Glazer alifikia makubaliano ya kununua hisa za wawili hao
McManus na Magnier ambayo ilimpa asilimia 60 ya umiliki.
Na mwishoni mwa majira ya joto mwaka huo huo Familia ya Glazer ilichukua umiliki
kamili wa miamba hiyo ya soka nchini England. Licha ya mafanikio ya uwanjani ya
klabu hiyo ya kutwaa mataji matatu ya ligi kuu na moja la ligi ya mabingwa
barani Ulaya kati ya mwaka 2007 na 2009 lakini umiliki huo uliwagharimu sana
Glazer ambapo kufikia mwaka 2010 deni ilikuwa limefikia pauni milioni 716.5
Ilifikia wakati mashabiki na wapenzi wa Manchester United walianza kwenda
kinyume na familia hiyo kwani Manchester United ilikuwa katika hali mbaya ya
kiuchumi.
Mashabiki hao walitaka aletwe mmiliki mwingine na pia walidai klabu ilirudi
katika rangi zake za asili za kijana na dhahabu.
Walienda mbali zaidi wakitaka hata jina lilirudi la zamani la FC United of
Manchester. Hata hivyo kufikia mwaka 2016 deni hilo lilipungua hadi kufikia
pauni milioni 322.1 huku mapata yakifikia pauni milioni 133.8
0 Comments:
Post a Comment