Sunday, March 15, 2020

RCL 2020: Nyamongo ya Mara yaichapa Huduma ya Dar mabao 2-1

 Mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kituo cha Kilimanjaro baina ya Huduma ya Dar es Salaam na Nyamongo ya Mara umemalizika kwa Nyamongo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Mabao ya Nyamongo yalifungwa na nyota wake Shaban Misabilo katika dakika ya 29 na Edson Mturi aliyepigilia msumari wa mwisho katika dakika ya 58 baada ya Huduma kucharuka na kusawazisha katika dakika ya 51 kupitia kwa Haniu Maulid.

Kocha John Mhina wa Nyamongo amesema ni jambo zuri kuanza vema safari ya kutafuta nafasi ya kusonga mbele, na kuongeza kuwa huo ni mwanzo wa safari wataendelea kurekebisha makosa ili wafanye vizuri.

Kwa upande wake Kocha Paul Nyombi wa Huduma amesema kuchelewa kufika katika kituo kumewafanya wasianze vema kwani hawajapata muda wa kupumzika wakiwasili kituo hapo jana Machi 14, mwaka huu.

"Tumemiliki vizuri lakini uchovu umetufanya tusipumzike lakini nina hakkika bado tuna nafasi ya kufanya vizuri," amesema Kocha Nyombi.

Kikosi cha Huduma kiliundwa na; Rashid Tarimo, Rasuli Juma, Shaban Ibrahim, Issa Mpanda, Islam Hamza, Ahmed Meja, Isack Komba, Said Mohamed, Khamis Halifa, Haniu Maulid, Emmanuel Pius.

Wa Akiba; Shomar Aboubakar, Seleman Shaban, Mariki Hamad, Aboubakar Ramadhan, Hance Venance, Sudi Abdallah.

Kikosi cha Nyamongo kiliundwa na; Yassin Ramadhan, Elias Yohana, Jembe Mkamba, Edson Mturi, Patrick Kate, Fredy Sululu, Emmanuel Athanas (C), Riziki Chaka, Shaban Misabilo, Benard Maranja, Maulid Mkonwa.

Wa Akiba; Hassan Robert, Bernado Mazigo, Fredy Mwita, Rajabu Lugembe, Pynethal Mguji, Yohana Shija.

STORY & PHOTO BY: Jabir Johnson
DATE: Machi 15, 2020






0 Comments:

Post a Comment