Machi 20, 1991 mabingwa watetezi wa Ulaya AC Milan walikataa kumalizia dakika mbili za mchezo wao wa robo fainali dhidi ya Olympique Marseille.
Katika mchezo wa kwanza waliochezea jijini Milan walitoka sare ya 1-1 baada ya majuma mawili Rossoneri walitua katika dimba la Velodrome.
Mchezo huo ulichezeshwa na mwamuzi Bo Karlsson kutoka Sweden ambaye aliotoa adhabu ya kadi za njano tatu kwa Milan na mbili kwa Marseille.
Kipindi cha kwanza kilimalizika bila kuona wavu ukitikisika pande zote mbili.
Katika dakika ya 75 ya mchezo winga wa Marseille Chris Waddle alivunja kitasa cha wageni hao kutoka Italia nakuipa uongozi klabu yake. Zikiwa zimebaki dakika mbili taa za Uwanjani hapo zilizimika na zikarudi baada ya dakika 15.
Mkurugenzi wa Milan wakati huo Adriano Galliani alikataa kurudisha timu uwanjani akitaka mechi ya marudiano ifanyike huku akisema watu wa televisheni ndio waliocheza mchezo huo kwani waliingia uwanjani.
Hata hivyo baadaye Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA) liliipa ushindi Marseille, huku AC Milan wakisimamisha kushiriki mashindano hayo kwa mwaka mmoja na pia walimfungia Galliani kujihusisha na soka hadi Julai 1993.
Marseille ilishindwa kutwaa taji hilo ikipoteza kwa changamoto ya mikwaju ya penati dhidi ya Red Star Belgrade ya Yugoslavia ya zamani katika mchezo uliochezwa San Nicolla, mjini Bari Italia Mei 29, 1991.
Marseille ilishindwa kufurukuta huku Red Star Belgrade ikiitwaa taji hilo kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo kwa mikwaju 5-3 ya penati mbele ya watazamaji 51,587.
0 Comments:
Post a Comment