Machi 21, 1980 alizaliwa mchezaji wa soka wa Kimataifa na mshindi mara
mbili wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia ya Shirikisho la Soka la Kimataifa
(FIFA) Ronaldo de Assis Moreira maarufu Ronaldinho Gaucho.
Ronaldinho alizaliwa Porto Alegre nchini Brazil. Aliitwa Ronalinho ikiwa na
Ronaldo Mdogo. Katika maisha yake ya soka aling'ara sana barani Ulaya akitwaa
mataji ya ligi na ligi ya mabingwa barani Ulaya akiwa na Barcelona na pia Kombe
la Dunia akiwa na Brazil.
Alianza maisha yake ya soka akiwa na klabu yake ya Gremio akiiungana na
kaka yake Roberto mnamo mwaka 1998.
Akiwa na kiungo mshambuliaji Ronaldinho alifunga mabao 21 ya ligi akiwa na
Gremio kati ya mwaka 1998 na 2001 kabla ya kutua nchini Ufaransa katika klabu
ya Paris St. Germain (PSG).
Alitua kkwa miamba hiyo ya Ufaransa kwa kitita cha euro milioni 5.1
Alitulia na PSG kwa misimu miwili mfululizo.
Akiwa huko alikutana kocha Luis Fernandez ambaye alimwona kuwa ni mchezaji
mzuri lakini akipendelea zaidi maisha ya anasa kuliko mpira.
Hata hivyo akiwa na PSG alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Brazil waliobeba
Kombe la Dunia mnamo mwaka 2002 lililofanyika nchini Korea Kusini na Japan.
Kucheza na kutwaa Kombe la Dunia ilikuwa ni hatua kubwa sana kwa nyota huyo
kwenye maisha ya soka. Alitoa mchango mkubwa katika mchezo wa robo fainali
dhidi ya England, wakati Brazil ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Hata hivyo alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika nane kabla ya mchezo huo
kumalizika hivyo alikosa nusu fainali. Ronaldinho alipata nafasi tena katika
mchezo wa fainali dhidi ya Ujerumani walipoibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Katika majira ya joto ya mwaka 2003, Ronaldinho aliondoka nchini Ufaransa
na kwenda Hispania katika jimbo la Katalunya kwa miamba ya soka ya Barcelona
kwa kitita cha euro milioni 32.3
Akiwa huko alikuwa miongoni mwa nyota akitwaa taji la Ligi Kuu nchini
Hispania (La liga) mnamo msimu wa 2004-05 na 2005-06 pia mwka 2006 alitwaa taji
la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Tuzo za mchezaji bora wa dunia alizitwaa mnamo mwaka 2004 na 2005.
Julai
2008 aliachana na Barcelona na kutua zake AC Milan ya Italia, na mnamo mwaka
2011 alirudi nchini Brazil katika klabu ya Flamengo baadaye Mineiro kisha
litimkia zake Mexico katika klabu ya Queretaro.
0 Comments:
Post a Comment