Mabingwa
watetezi wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya Liverpool wameondolewa katika kinyang’anyiro
hicho baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Atletico Madrid kwenye
mchezo uliochezwa Anfield.
Katika
mzunguko wa kwanza wa hatua ya 16 jijini Madrid Liverpool ilizabuliwa kwa bao
moja hivyo miamba hiyo imetolewa kwa uwiano wa mabao 4-2.
Katika
mchezo huo mabao ya Marcos Llorente (97’, 105’) na Alvaro Morata (120’)
yalitosha kuwaondoa mabingwa hao mara saba wa taji hilo.
Bao la
dakika ya 43 la Georgio Wijnaldum halikutosha kumwokoa Jurgen Klopp na kichapo
hicho.
Rojiblancos
wanakuwa timu ya kwanza kuvunja rekodi iliyokaa miaka mingi ya Liverpool
kutandikwa nyumbani. Mara ya
mwisho kuzabuliwa katika dimba hilo ilikuwa Oktoba 2014 ambapo miamba ya
Hispania Real Madrid iliweka rekodi hiyo.
Rekodi ya
Liverpool katika dimba hilo ni kwamba katika mechi 25 za barani Ulaya imeshinda
mara 18 na kutoa sare 7.
0 Comments:
Post a Comment