Kamati ya Olimpiki ya kimataifa (IOC) imethibitisha kuwa michezo ya Olimpiki Tokyo 2020 inaahirishwa hadi mwakani kwa sababu ya janga la ugonjwa wa corona uliotikisa dunia kwa sasa.
Michezo hiyo ilitakiwa kuanza kufanyika Julai 24, 2020, lakini sasa imesogezwa mbele hadi mwakani 2021.
Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe amesema wamekubaliana kuahirisha kwa mwaka mmoja na rais wa IOC, Thomas Bach amekubali kwa asilimia 100%.
Pia, Michezo ya Tokyo Paralympic imesogezwa mbele hadi 2021. Michezo hiyo itaendelea kuitwa Tokyo 2020 pamoja na kuwa itafanyika 2021.
Katika taarifa ya pamoja kati ya waandaji wa Tokyo 2020 na IOC ilisema kumetokea jambo ambalo hakuna aliyetegemea kuona namna ugonjwa huu unavyosambaa kwa kasi duniani kote.
Olimpiki haijawahi kuahirishwa tangu kuanzishwa kwake miaka 124 iliyopita, japokuwa haikufanyika mwaka 1916, 1940 na 1944 kwa sababu ya vita viwili vya dunia.
Wakati wa vita baridi baadhi ya nchi ziligomea kushiriki mashindano ya Moscow na Los Angeles kati ya mwaka 1980 na 1984.
CHANZO: CRI Swahili
0 Comments:
Post a Comment