Serikali imetenga
kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya kujenga mradi mkubwa wa maji kutoka
Ziwa Chala ili kutatua changamoto ya majisafi na salama inayowakumba wakazi wa
vijijini katika wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro.
Akiwa mjini Moshi katika
ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa upanuzi wa mtandao wa maji safi wenye
jumla ya urefu wa mita 2,724, unaotekelezwa na Mamlaka ya majisafi na Usafi wa
Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa alisema Serikali
imeanza utekelezaji wa mradi huo ambapo tayari imeshakamilisha utafiti wa
awali na kuainisha maeneo yanayofaa kwa ujenzi huo ili wananchi wa wilaya ya
Rombo waweze kupata huduma hiyo ya maji.
Alisema huo utaenda
kwa awamu tofauti totafuti, ambapo Wataalamu wa MUWSA kwa
kushirikiana na Wataalamu wa Malamlaka ya Maji Vijijini na Mjini (RUWSA).
“Naipongeza Mamlaka ya
Maji Usafi na Usafio wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA), kwa kazi nzuri
inayoifanya ya kuhakikisha wananchi wanapata majisafi na salama, napenda kusema
kwenye maeneo ya mjini upatikanaji wa maji safi na salama uko vizuri,
changamoto iliyopo ni kwenye maeneo ya vijijini,”alisema.
Awali akitoa taarifa
yake kwa Waziri, Kaimu mkurugenzi wa
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (MUWSA) Mhandisi Aron Joseph, alisema
Mamlaka inatekeleza ujenzi wa upanuzi wa mtandao wa Maji Safi wenye jumla
ya urefu wa mita 2,724.
“Mradi huu
umelenga kuondoa changamoto ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama
lililokuwepo kwa muda refu katika kata ya Kimochi kwenye eneo la Kiraracha,
Kitonyi na eneo la Kitonyi hadi Sango,”alisema mhandisi Joseph.
Alisema kukamilika kwa
mradi huo utagharimu kiashi cha takriban ya Sh milioni
101,172,100 ambapo jumla ya kaya 3,307 zitanufaika na mradi huo.
“Mradi unatekelezwa
kwa awamu mbili , eneo la Kiraracha hadi Kitonyi na eneo la Kitonyi hadi
Sango, ambapo hatua za utekelezaji wa mradi huo umekamilika kwa asilimia 100,
huku eneo la Kitonyi hadi Sango hatua za utekelezaji wa mradi huo umefikia
asilimia 95,”alisema.
Nae Kaimu meneja
Ufundi Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (MUWSA) Mhandisi Kija Limbe,
alisema kuwa mamlaka hiyo inatoa huduma ya majitaka kwa asilimia 31 ya wakazi
wote wa Manispaa ya Moshi, yenye wakazi wapatao 205,113.
Alisema mabwawa ya
majitaka yamesanifiwa kupokea mita za ujazo 4,500 kwa siku ambapo hali ya
mabwawa hayo kwa sasa yanapokea kiasi cha mita za ujazo 4,300 kwa siku
kutoka kwenye mtandao wa majitaka uliopo.
“Jumla ya mita za
ujazo 16,170 kwa siku za majitaka zinakadiriwa kuzalishwa ndani ya mji wa
Moshi,”alisema.
Aidhi alisema
changamoto iliyopo kwa sasa ni mabwawa ya majitaka kukaribia kufikia uwezo wake
wa mwisho wa kupokea majitaka ambao ni mita za ujazo 4,500,”alisema Mhandisi
Limbe.
Jabir Johnson akiripoti kutoka Ziwa Chala, Rombo mkoani Kilimanjaro |
Ziwa Chala linavyoonekana kwa karibu |
STORY
& PHOTO BY: Kija Elias, Jabir Johnson
EMAIL:
eliaskisena@gmail.com
DATE:
Machi 4, 2020
0 Comments:
Post a Comment