Machi 12, 417 alifariki dunia kiongozi mkuu wa Kanisa
Katoliki Papa Innocent I.
Alifariki dunia baada ya kukalia wadhifa huo kwa miaka
16. Alianza kuongoza kanisa hilo Desemba 22, 401. Baada ya kifo chake Papa
Zosimus alishika nafasi yake.
Aliyempokea hakukaa sana alifariki dunia baada ya mwaka
mmoja na huo ulikuwa mwaka 418. Tangu kuingia kwake katika viunga vya Vatican
alikuwa mpatanishi mkuu wa mizozo ya kikanisa.
Pia alithibitisha hakimiliki ya Askofu Mkuu wa
Thesalonike, na akatoa uamuzi wa kushughulikia mashauri ya kinidhamu ambayo aliletewa
na Askofu wa Rouen.
Alitetea uhamishwaji wa John Chrysostom ambaye alikuwa Askofu
Mkuu wa Konstantinopo na kushauriana na maaskofu wa Afrika juu ya ubishi wa
WaPelagian, akithibitisha maamuzi ya maelewano ya Kiafrika.
Miaka ya 1500, Mchungaji Mkatoliki-msomi Johann Peter
Kirsch, miaka 1500 alimuelezea Papa Innocent kama mtu mwenye nguvu na mwenye
kipawa "... ambaye alitimiza majukumu yake aliyoyapenda katika ofisi yake."
Kwa mujibu wa mwandishi wa biografia katika Liber
Pontificalis ambacho ni kitabu cha Mapapa wa kanisa hilo kutoka kwa Mtakatifu
Petro hadi karne ya 15, Papa Innocent alikuwa mtu wa Albano Laziale na mtoto wa
mtu anayeitwa Innocentius, lakini wakati wake Jerome alifuata nyayo kama mwana
wa papa wa zamani, Anastasius I, Anastasius I alikuwa papa wa Kanisa Katoliki
kutoka Novemba 27, 399 hadi kifo chake mwaka 401 ambapo alipokea Papa Innocent.
Kulingana na Urbano Cerri, Papa Innocent alikuwa raia wa
Albania.
Papa Innocent I hakupoteza nafasi yoyote katika kudumisha
na kupanua mamlaka ya Kitume kwa Warumi, ambayo ilionekana kama njia ya mwisho
ya kusuluhisha mabishano yote ya kidini.
Mawasiliano yake na Victricius wa Rouen, Exuperius wa
Toulouse, Alexander wa Antiokia na wengine, pamoja na hatua zake juu ya rufaa
aliyopewa na John Chrysostom dhidi ya Theophilus wa Alexandria, zinaonyesha
kuwa fursa za aina hii zilikuwa nyingi na tofauti.
Alichukua maoni yaliyoamua juu ya mzozo wa Pelagian,
akithibitisha maamuzi ya sinodi ya mkoa wa kiafrika, uliyofanyika Carthage
mnamo 416, akithibitisha hukumu hiyo ambayo ilitamkwa mnamo 411 dhidi ya
Cælestius, ambaye alishiriki maoni ya Pelagius.
Mara tu baada ya hii, maaskofu watano wa Kiafrika, kati
yao Mtakatifu Augustine, waliandika barua ya kibinafsi kwa Papa Innocent I
kuhusu msimamo wao katika suala la Uhamaji.
Mwanahistoria Zosimus katika Historia Nova aliandika
kwamba wakati mji wa Rome ulipotekwa na watu kutoka Ujerumani mnamo Agosti 24,
410 katika mapambano yaliyoongozwa na Mfalme Alaric I.
Papa Innocent I tayari tayari kuruhusu mazoea ya kipagani
ya kibinafsi kama hatua ya muda.
Kwa wakati huo Rome haukuwa mji mkuu wa Dola la Rumi
kwani mwaka 286 makao makuu yalikwenda Mediolanum ambayo kwa sasa ni Milan na
mwaka 402 makao makuu yalikuwa Ravenna kaskazini mwa Italia.
Hata hivyo mwandishi huyo wa Historia Nova alisema
jaribio la wapagani la kurejesha ibada ya umma lilishindwa kwa sababu ya
ukosefu wa masilahi ya umma, ikionesha kwamba Roma ilikuwa imefanikiwa katika
Ukristo wake katika karne moja iliyopita.
Hakuna tarehe inayoonyesha alizaliwa lini lakini Papa
Innocent anatajwa kuwa alizaliwa huko Albano ukiwa ni umbali wa kilometa 15
kutoka Rome. Pia mwaka aliozaliwa Papa Innocent I haujawekwa bayana wala miaka
yake aliyoishi hadi kufa kwake.
0 Comments:
Post a Comment