Saturday, March 28, 2020

Mwanamuziki wa Reggae Delroy Washington afariki dunia kwa Covid-19



LONDON, ENGLAND
Mwanamuziki mahiri wa Reggae Delroy Washington amefariki dunia jijini London, Uingereza. Nyota huyo wa muziki ambaye jina lake halisi ni Delroy Washington amefariki dunia wakati ambao fani ya muziki huo ikiwa na uhitaji naye. 

Mwanamuziki huyo amefariki dunia kwa maambukizi ya virusi vya Covid-19. Katika akaunti ya Instagram ya mwanamuziki Winston Francis @ winstonmrfixitfrancis aliandika kuelezea machungu ya kumpoteza rafiki yake na mkali wa muziki wa reggae kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

The Voice imethibitisha kuondokewa na mwanafamilia huyo katika medani ya muziki wa Reggae. 

Alizaliwa mnamo mwaka 1952 Westmoreland nchini Jamaica na familia yake ilihamia nchini Uingereza wakati akiwa mtoto miaka ile ya 1960.

Alianza muziki akiwa meneja wa kuratibu ziara na mara chache katika vipindi vya muziki katika bendi ya Rebel. Wakati alipoingia kikamilifu katika uimbaji alikuwa solo akirekodi na Count Shelly na baadaye akimsaidia Bob Marley  na The Wailers katika albamu mbalimbali.

Alikuja kuwa rafiki wa karibu wa waimbaji maarufu miaka ya 1970 na baadaye aliwavutia wengi nchini Uingereza kutokana na mistari katika nyimbo zake. Mnamo mwaka 1976 alitoa albamu yake I Sus na mwaka 1977 alitoa albamu iliyofahamika kwa jina la Rasta.

Pia alishiriki katika baadhi ya singo ikiwamo ile ya Likes of Jah Shaka. Mbali ya mchango wake mkubwa katika muziki alileta mabadiliko makubwa alipofanikiwa kuwa mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa Shirikisho la Muziki wa Reggae nchini Uingereza ambako alifanya kampeni ya kutambuliwa kwa London Borough huko Brent kama makao makuu ya Muziki wa Reggae nchini Uingereza na Ulaya kwa ujumla.

Lebo za muziki huo kama Island Records na Jet Star zilikuwa zikifanya kazi kutokea hapo. 

Hata hivyo Delroy anasalia katika vichwa vya wengi kwa alikuwa miongoni mwa wanaharakati wa kijamii ambaye aliendeleza kazi nzuri zikiwamo 12 Tribes of Israel, HPCC Bridge Park or I & I Idren of Israel.

Hakika upole wake, ubunifu na roho yenye akili na umakini itakosekana miongoni mwa wapenzi na mashabiki wa muziki wa reggae.


STORY & PHOTO BY: Jabir Johnson
EMAIL: jabirjohnson2020@gmail.com
DATE: Machi 27, 2020
Singles
"Jah Man a Come" (197?), Lord Koos
"Lonely Street" (1973), Count Shelly
"Papa Was a Rolling Stone" (1973), Sir Christopher
"Freedom Fighters" (1976), Axum
"Give All the Praise to Jah" (1977), Virgin - 12-inch
"Memories" (1978), Burning Sounds - Delroy Washington & Jah Son
"It's Like Magic" (197?), Burning Vibrations - 12-inch
"Magic" (1980), Direction Discs/Ballistic - Delroy Washington Band
"Cool Rasta" (19??), Ballistic
"For Your Love" (1981), Ankh/Pinnacle

0 Comments:

Post a Comment