Saturday, March 21, 2020

Ifahamu Nyota Yako


Unajimu au astrolojia ni elimu juu ya uhusiano kati ya nyota na maisha ya binadamu duniani. Wanazuoni wa unajimu wanaeleza ya kwamba nyota zinaathiri maisha ya watu na matukio kama amani, vita au maafa. 

Mahusiano haya hayajaweza kuthibitishwa na sayansi ya fizikia au sayansi nyingine. Alama za nyota 12 ni msingi wa falsafa hii ya unajimu. Astrolojia imekuwa ikitumika kwa miaka mingi lakini siku zote imekuwa ikipata upinzani mkubwa toka kwa wana sayansi. 

Astrolojia ina misingi tokea enzi za zamani wakati sayansi ilipokuwa ya chini na imani za kiroho na kiungu zikiwa za kiwango cha juu katika jamii nyingi. Baadhi ya tafiti zilizofanywa kuchunguza usahihi wa astrolojia unaonyesha kuna usahihi wa asilimia kama 30 tu. 

Hata hivyo Astrolojia inapata upinzani mkubwa ulimwengu wa sayansi ya kisasa.

Samaki (Pisces):Feb 19 – Machi 20
Kondoo (Aries): Machi 21 – Aprili 19
Ng’ombe (Taurus): Aprili 20 – Mei 21
Mapacha:(Gemini ): Mei 22 – Juni 20
Kaa(Cancer): Juni 21 – Julai 22
Simba(Leo): Julai 23 – Agosti 22
Mashuke(Virgo):Agosti 23 – Sept 22
Mizani (Libra): Sept 23 – Okt 22
Ng’e (Scorpio): Okt 24- Nov 21
Mshale (Sagittarius): Nov 22- Des 21
Mbuzi(Capricorn):Des 22 – Jan 19
Ndoo (Aquarius):Jan 20 – Feb 18

0 Comments:

Post a Comment