Tahadhari imeendelea
kuchukuliwa katika makampuni mbalimbali kuhusu kusambaa kwa virusi vya
Covid-19 ambapo Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Bonite Bottlers mjini Moshi, Kilimanjaro
imekuwa miongoni mwa washiriki wa mwanzo kuchukua tahadhari hiyo katika eneo la
kiwanda hicho kwa kuweka vifaa mbalimbali vikiwamo dawa za kunawia mikono kwa
ajili ya wafanyakazi wake na kile anayeingia humo.
Haya yanajiri ikiwa
ni siku baada ya mgonjwa wa Covid-19 kubainika jijini Arusha na kuletwa katika
Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi mjini Moshi.
Akizungumza katika
hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Shindano la V.I.P Club 2019
iliyofanyika kiwandani hapo Meneja Mauzo wa Bonite Bottlers Arusha Boniface
Mwassi alisema kutokana na tukio lililotokea jijini Arusha hawana budi kuchukua
tahadhari zote kwa ajili ya usalama wa wafanyakazi na wateja.
Wateja 25
waliojishindia pikipiki kutoka Manyara, Karatu, Singida, Arusha na Kilimanjaro wamekabidhiwa
zawadi zao na kuondoka nazo.
Wateja wengine 18
waliojishindia kreti 50 na 100 za soda walikuwa miongoni mwa waliokabidhiwa
zawadi zao katika hfala hiyo.
0 Comments:
Post a Comment