Monday, March 2, 2020

Ufahamu mwezi Machi

Machi ni mwezi wa tatu wa mwaka ambao ulitapewa jina hilo badala ya Mars katika kalenda za Julian na Gregori. 

Ni mwezi wa pili katika miezi saba yenye siku 31. Katika mzingo wa kaskazini wa dunia ni mwanzo wa vipindi vya joto. 

Hata hivyo inapofika Machi 20 au 21 hali ya hewa dunia huwa sawa ambapo usiku na mchana unakuwa sawa. Pia tarehe hizo ni kiashirio kuwa mwanzo wa majira ya joto katika mzingo wa kaskazini na mwanzo wa majira ya baridi katika mzingo wa kusini wa dunia.

Asili ya mwezi Machi ilitoka na jina Martius  ambao ulikuwa ni mwezi wa kwanza katika kalenda ya kale ya Kirumi. 

Jina hilo ulipewa mwezi huo kutokana na Mars ambaye alikuwa Mungu wa Vita wa Warumi ambaye alikuwa na watoto Romulus na Remus kwa Warumi hao wa kale. 

Mwezi huo ulikuwa mwanzo wa msimu wa vita na sikukuu lakini kwa heshima sikukuu waliamua kuziweka mwezi Oktoba. 

Wanahistoria wanasema mwezi Machi ulisalia kuwa mwezi wa kwanza hadi mwaka 153 K.K na sikukuu nyingi zilizokuwepo katika mwezi huu zilikuwa zinaashiria kuanza kwa mwaka mpya baada ya kipindi cha baridi.

 Katika ardhi ya Finland mwezi huu huwa wanauita Maaliskuu ukiwa ni mwezi ambao ardhi inaanza kuonekana baada ya theluji iliyofunika kuondoka. Ni muda ambao ni wa machipuko, kilimo huanzia hapo.



0 Comments:

Post a Comment