Friday, March 27, 2020

Ujio wa Dkt. Mwakyembe kwa Wanahabari Kilimanjaro

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harisson Mwakyembe akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro Januari 24, 2020. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini Kippi Warioba. (Picha zote na Jabir Johnson)


Januari 24, 2020 mkoa wa Kilimanjaro ulipokea ugeni mkubwa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambao ulikuwa na madhumuni ya kuzungumza na waandishi wa habari mkaoni humo. 

Ugeni huo uliongozwa na Dkt. Harisson Mwakyembe ambaye alipata fursa ya kuzungumza na wanahabari hao kutoka vyombo vyao wanavyofanyia kazi. Miongoni mwa masuala aliyoyazungumza mbele ya waandishi wa habari hao kuwa amezunguka nchi nzima na kujionea namna ambavyo waliopo kwenye tasnia hiyo wapo katika hali ya unyonge ambao umechangiwa na masuala mbalimbali. 

Miongoni mwa unyonge huo ni kudharauliwa kwa wanahabari licha ya kazi kubwa wanayoifanya kwa jamii kwani imekuwa ikichukuliwa kuwa tasnia ya watu wasiostahili na ndio sababu kipato chao kimekuwa cha chini hali inayowafanya waishi kiunyonge.

Pia katika kikao hicho muhimu Dkt. Mwakyembe aliongoza na ujumbe kutoka wizarani. Pia uwepo wa Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini Kippi Warioba, Uwepo wa Mkurugenzi Mtendaji wa TBC Ayub Rioba. Mbali na hilo kulikuwapo uongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Kilimanjaro (MECKI) chini ya Mwenyekiti wake Bahati Mustapha Nyakiraria ambaye aliwasili ujumbe wa wanahabari hao mbele wa Dkt. Mwakyembe.









0 Comments:

Post a Comment